Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazngira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na
maafisa na waaandishi wa habari alotangulizana nao katika DAMPO la mji wa
Tabora na kushangazwa na hali halisi ya DAMPO hiyo na taarifa ya mazingira
aliyopewa na mkoa kuhusu usafi wa mazingira wa mji wa Tabora
Bw.
Benjamini Dotto Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi
wa mazingira NEMC (katikati) akieleza kitaalam nini kifanyike katika DAMPO la
Mji wa Tabora kabla ya manispaa kuwasilisha mpango mkakati kuhusu dampo la mji
huo. (Picha na Evelyn Mkokoi)
Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina ameipa adhabu Halmashauri ya Maispaa ya Mji wa Tabora kwa kuitoza faini
ya shilingi Milioni kumi na mbili na kutakiwa kulipa faini hiyo kwa muda wa
wiki mbili, kwa kile kilichodaiwa ni kutokutii mamlaka za juu na kusema uwongo
kuhusu hali ya usafi wa maingira ya mji wa Tabora.
Alipokoukuwa katika siku ya Pili ya ziara yake mkoani Tabora
baada ya kupata taarifa ya hali ya mazingira ya mkoa huo, Na kuambiwa kuwa ni
ya kuridhisha na kuwa DAMPO la mji huo ambalo siyo rasmi,lipo katika hali ya
kuridhisha ndipo alipoamua kjutembelea DAMPO hilo na kujioea hali ya uchafu
isiyovumilika kwa taka ngumu na hatarishi, kutomwagwa katika eneo husika na
kuzagaaa barababarani.
Aidha kufuatia malalamiko ya wakazi wa mji huo, Mpina halikadhalika
aliktembelea soko ya mji wa Tabora na kushuhudia Dampo katikati ya soko hilo
lenye taka mbichi zenye harufu kali ambayo huweza kuhatarisha maisha ya watumiaji
wa soko hilo kwa kupata magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Bw. Bosco
Nduguru alisema ofisi yake ilikuwa na mpango wa kuhamishia soko hilo sehemu
nyingine na kukubali changamoto zilijitokeza sokoni hapo na kuzifanyia kazi
wakati mwenyekiti wa soko hilo bwana Bakari Mpumila alieleza kuwa kuhamishwa
kwa soko hilo hakuwezi kuwa suluhisho la kudumu kutatua changamoto za usafi wa
mazingira kwani dampo linalotumika katikati ya soko hilo limekuwa ni kero
iliyoshindikana toka kwa uongozi uliopita na Kumshukuru Naibu Waziri Mpina kwa
ziara yake kwani ana imani kuwa sasa kero hiyo imeshatapatiwa ufumbuzi wa
kudumu.
Pamoja na kulipa faini hiyo manispaa pia inatakiwa kuondosha
taka hizo a kumwaga kifisi cha molamu katika eneo hilo na kurekebisha mazingira
ya choo sokoni hapo.
0 comments:
Post a Comment