Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na: Mwandishi Wetu.
MUSWADA wa huduma za
Habari wa mwaka 2016 umeelezewa kuwa muarubani wa uandishi wa habari za
kughushi na uchochezi kutokana na kuwa na vifungu vyenye kumlinda mwandishi na
kumuweka hatiani pindi anapoenda kinyume na matakwa ya sheria.
Hayo yamebainishwa na
Mkurugenzi wa Kurgenzi ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC),
Bernard James wakati wa mahojiano maalum
na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es Salaam.
“Baadhi ya waandishi
wa habari wamekuwa na tabia za kandika habari za kughushi na mara nyingine
zenye lengo la kumkashfu mtu, ni imani yangu kwamba muswada huu ni muafaka kwa
watu kama hao”. Alisema Bernard.
Bernard alivitaja
vifungu hivyo kuwa ni Sehemu ya Tano ya muswada huo kuanzia kifungu cha 32 hadi
39 ambavyo vinahusu mambo ya kashfa ambapo mwandishi ana anayo haki yake, hali kadharika anao wajibu wa kuzingatia
misingi ya sheria na mipaka yake.
Huku sehemu ya saba
ikihusisha makosa mbalimbali yakiwemo uchochezi,habari za kuchochea uasi, makosa
yanayohusu utangazaji, vyombo vya habari na kosa la habari za kutia hofu kwa
jamii.
Alisema kuwa ni vyema
wanahabari wakatambua kwamba Serikali imeleta muswada huo si kwa nia ya
kukandamiza uhuru wa habari bali ni nia yake yakutaka kuona kunakuwa na
maboresho katika tasnia ya hii na siyo
kama ambavyo wengi wao wamekuwa wakipotosha.
Aidha Bernard
aliongeza kuwa muswada huo ukipitishwa utapelekea kuanzishwa kwa chombo
kitakachosimamia waandishi wa habari kwa kuwapa Vitambulisho, kusimamia maadili na mienendo ya taaluma za waandishi
wa habari na kuongeza kuwa tasni itaheshimika kwani wale makanjanja hawatakuwa
na nafasi tena.
“Binafsi naunga mkono
muswada huu upitishwe ili tasnia ya habari iheshimike kama taaluma nyingine
zinavyoheshimika”.Aliongeza.
Amewaomba wanahabari
wenzake kuunga mkono Muswada huu unaotarajiwa kusomwa Bungeni kwa mara ya pili
siku ya Ijumaa ya tarehe 4 Novemba ambapo utajadiliwa na kupitihwa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment