Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
Serikali
ya Mkoa wa Tabora imetoa siku mbili kwa Halmashauri tatu za Mkoa huo
kuhakikisha wanatimitiza ahadi zao za kuwalipa fedha au kutoa zawadi kwa
wanyakazi bora waliochaguliwa katika kilele cha sherehe za mwaka 2016.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati
wa kilele cha sherehe za Mei Mosi kwa ngazi ya Mkoa huo.
Hatua
hiyo ya Mkuu wa Mkoa imefuatia malalamiko yalitolewa kuhusu Halmashauri
ya Igunga, Nzega Mjini na Manispaa ya Tabora kutowalipa wafanyakazi
bora waliochaguliwa mwaka 2016 wakati Shirikisho la Vyama Huru vya
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) liliposoma risala yake.
Alisema
kuwa ni vema Halmashauri zilizolalamikiwa zikatimiza ahadi hizo kwa
kuwa ni haki ya watumishi waliofanya vizuri ili kuwahamasisha waendelee
kufanya vizuri na wenzao waweze kuiga kwa ajili ya kuongeza ufanisi
sehemu zao za kazi.
Bw.
Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zilizotajwa kuhakikisha
zinawapa zawadi au kuwaandikia hundi washindi wa mwaka jana katika
maeneo yao na kuwalisha Ofisini kwake taarifa ya utekelezaji wa agizo
hilo ifikapo Jumatano asubuhi.
Alisema
kuwa hawezi kukubali Watendaji wawakatishe tamaa wafanyakazi
wanaojituma na kuwajibika kwa bidii zote katika maeneo yao ya kazi na
kuongeza kuwa ni vema wakapewa haki yao kama ilivyokubalika na kwa
mujibu wa taratibu.
Katika
risala yake TUCTA ilizitaja Halmashauri ya Nzega Mjini , Igunga,
Manispaa ya Tabora na Bodi ya Tumbaku Tanzania kuwalipa zawadi
wafanyakazi bora wa mwaka 2016 licha ya kuwaahidi.
Ilisema kuwa hali hiyo ni ubabaishaji na inakatisha tama kwa wafanyakazi wa meneo hayo.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora awaagiza kuhakikisha wanawalipa
haki zao zote watumishi wanapohamisha kutoka Halmashauri moja kwenda
nyingine kama kanuni na taratibu zinavyotaka.
Alisema
kuwa mtumishi anapoahamishwa anapaswa kulipwa hela ya usumbufu na
mwajiri wake wa awali na fedha za kujikimu yeye na familia yake na
mwajiri wake mpya.
Bw.
Mwanri alisema kuwa utekelezaji huo hauhitaji kiongozi juu ndiye aje
kufuatilia bali ni jukumu la Wakurugenzi kuhakikisha watekelezaji
taratibu hizo ili kuondoa kero sizo za lazima kwa watumishi hadi
walalamike.
Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment