Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Serikali imezindua mradi wa ujenzi na
usambazaji maji vijijini wenye thamani ya shilingi bilioni 29 katika
Halmashauri saba za mkoani Tabora.
Mradi huo umezinduliwa leo na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Kijiji
cha Mabama Wilayani Uyui mkoani Tabora.
Ujenzi wa Mradi huo umefadhiliwa na
Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ambao umewezesha uchimbaji
wa visima 111 na ujenzi wa mitandao minne ya bomba.
Akizungumza na wananchi wa Mabama
mkoani Tabora wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo Makamu wa Rais huyo
alisema kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuhakikisha
wananchi wengi hapa nchini na wale wa mkoa huo wanakuwa na uhakika wa huduma ya
maji safi na salama.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni
kuendelea na jitihada kuwajenga miradi mbalimbali wananchi kwa nguvu zake na
wakati mwingine kwa kushirikiana na wahisani.
Mhe. Samia alisema kwa kuwa mradi huo
utawanufaisha wanachi wapatao 40,352 katika vijijini 31 vya Mkoa wa Tabora ni
vema wananchi wakautunza ili uweze kutumika kwa muda mrefu.
Aliwaasa wanufaika wa mradi huo maji
vijijini kutoharibu miundo mbinu za visima na bomba ili uweze kusaidia
kuwaondolea adha wananchi na hasa wakinamama na watoto wa kike ambao walikuwa
wakitumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kushiriki katika shughuli
nyingine za uzalishaji mali.
Aidha , Makamu huyo wa Rais ametoa kwa
wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili jamii iendele kunufaika na
rasimali hiyo muhimu kwa uhai wa wanandamu na maendeleo mengine.
Aidha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano huyo ameishukuru serikali ya Japani kwa msaada huo ambao ni ukumbozi
kwa wakazi wa Tabora.
Hivyo kufuatia hali hiyo aliwaagiza
viongozi kuanzia ngazi ya chini hadi Mkoa kutomfumbia macho mtu anayeharibu
mazingira kwa makusudi na ikiwezekana hatua kali zoichukuliwe dhidi yake.
Naye Balozi wa Japani hapa nchini Mhe.
Masaharu Yoshida alisema kuwa Japan itandelea kushirikiana na Tanzania katika
ujenzi wa miradi mbambali hapa nchini kwa lengo la kuwaletea huduma wananchi
kwa karibuni.
Alisema kuwa ujenzi wa mradi huo ni
ishara ya ushirikiano mzuri uliopo mbaina ya Tanzania na Japan na kuahidi kuendelea
na ushirikiano huo.
Awamu Mkuu Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey
Mwanri alitoa salamu za Mkoa alisema kuwa uharibifu wa mazingira mkoani huo kwa
sababu za kilimo cha tumbaku kisichozingatia matumizi madogo ya kuni na ufugaji
wa usiozingatia utunzaji wa mazingira umesababisha upungufu wa mvua mkoani huo.
Alisema kuwa wakati mazingira mkoani
bado hayajaharibiwa mkoa huo ulikuwa na uwezo wa kupata mvua kufikia milimita
1800 lakini hivi sasa Tabora inapata mvua ambazo ni milimita 650.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema
kuwa ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa Mazingira, viongozi mbalimbali
wa mkoani huo wameendesha kampeni ya kupata miti katika maeneo yote kwa kutumia
teknolojia ya matone.
Naye Waziri wa Maji na Uwagiliaji
Greyson Lwenge alitoa wito kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote hapa
nchini kuanzisha miradi ya uchumbiaji wa mabawa madogo madogo kwa ajili ya
kukabiliana na tatizo la maji katika maeneo yao.
Alisema kuwa Wizara hiyo itaendelea na
jitihada zake za utatizi wa kero ya maji , lakini vema na Halmashauri zitafuta
njia za kuwaondolea wananchim kero hiyo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Uyui Said Shaban alisema kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwa baadhi ya
wakazi wa mkoa wa Tabora na hasa Halmashauri yake kwa kuwa walitumia muda
mwingi na fedha nyingi kununulia maji.
Alisema kuwa baada kujengwa mradi huo
hivi sasa wananchi wananunua dumu moja la lita ishirini kwa shilingi 50 wakati
hapo awali walikuwa wakinunua kwa kiwango cha kuanzia shilingi 500 hadi 1,000
wakati wa kiangazi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mradi huo
pia umesaidia kupunguza muda mwingi ambao wakinamama waliupoteza kutafuta
maisha badala ya kwenda kuzalisha mali.
Aliongeza kuwa faida nyingine ni kuwa
mradi huo umesaidia kurudisha mahusiano katika familia.
0 comments:
Post a Comment