Na Tiganya Vincent-RS-Tabora.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia
kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika
kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora.
Taarifa
hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye
pia ni Mkuu wa Wialaya ya Tabora Queen Mlozi imesema kuwa sherehe za
uzinduzi wa mradi huo zitaanza asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe 29
Mwezi huo.
Amesema
kuwa baada ya uzinduzi wa mradi huoi , Makamu wa Rais atapata fursa ya
kuwahutubia wananchi na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Shule ya
Msingi Mabama.
Aidha ,
Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa viongozi wa dini zote,
vyama vyote vya siasa, viongozi wa serikali na wananchi wa maeneo
yaliyopo karibu na mradi huo kujitokeza kwa wingi kwenda kusikiliza
hotuba ya Makamu wa Rais.
Uzinduzi
wa mradi huu utasaidia kuondoa tatizo la maji safi na salama kwa wakazi
wa eneo hilo na ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaondole
matatizo mbambali wananchi likiwemo la upatikanaji wa maji safi na
salama.
Mradi huo
wa maji ambao umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Japan(JICA) umewezesha umesaidia uchimbaji wa visimana ujenzi mitandao
ya mabomba katika eneo hilo wilayani Uyui.
0 comments:
Post a Comment