Tiganya Vincent, RS-Tabora
Wananchi
wa Mkoa wa Tabora wanaokwenda kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa Kitete wameondokana na adha ya muda mrefu ya kunyeshewa mvua na
kukaa juani baada ya kukamilika na kuzinduliwa kwa Jengo la Mahali pa
Kungonjea kuona wagonjwa.
Jengo hilo lililojengwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora na umegharimu shilingi milioni 18 hadi kukamilika.
Uzinduzi
huo umefanywa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi wakati wa
sherehe fupi zilzofanyika katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa huo Kitete.
Alisema
kuwa kukamilika kwa jengo hilo kwa muda kumesaidia kuondoa kilio cha
muda mrefu cha viongozi na wananchi cha kutaka lijengwe eneo la watu
kupumuzika wakati wakisubiri muda wa kuona wagonjwa wao wanapata
matibabu katika Hosptali hiyo.
Kaimu
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliipongeza Seketarieti ya Mkoa wa Tabora
kwa kuwa wabuni hadi kufanikisha ujenzi huo kwa kiwango cha juu na
gharama nafuu.
Naye
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alisema kuwa ujenzi wa
jengo hilo umefanywa kwa kutumia fedha za usimamizi wa miradi ambapo
Seketarieti ya Mkoa huo imepunguza katika fedha zake za kufuatilia
miradi.
Alisema
kuwa hatua hiyo imesaidia kupatikana kwa fedha hizo zilizosaidia
kukamilisha kwa jengo ambalo ambalo litasiadia kuepusha wananchi hao na
hatari za kugongwa na baiskeli au pikipiki kutokana na kukaa kando kando
ya barabara.
Katibu
Tawala huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kabla ya ujenzi huo walitaka
kumtumia Mhandisi kutoka nje ambapo alidai apatiwe shilingi milioni 35
ili afanikishe ujenzi huo , lakini walipoamua kutumia mwandishi wa ndani
wameokoa kiasi cha milioni 17.
Aidha
, Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa Wakurugenzi wote
Watendaji wa Halmashauri nane(8) za mkoani Tabora kuhakikisha wanajenga
jengo kwa kila Hospitali la Mahali pa wananchi kuongejea kuona wagonjwa
wao.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuwaondelea kero wananchi na kutekeleza ahadi
ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwajali wanyonge.
Aidha
, Dkt. Ntara aliwaahidi wananchi kuwa baada ya kukamilika kwa jengo
hilo atajitadi kuwanunulia runinga ili wanapokuwa wanasubiri kuona
wagonjwa wafutilie taarifa mbalimbali za habari zinaendelea za ndani na
nje ya nchi.
Katika
hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora wanatarajia kujenga
Kliniki mbili katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete kwa
ajili ya vijana na wakinamama.
Alisema
kuwa lengo la kutaka kufanya hivyo ni kutaka kutoa elimu kwa vijana
hasa mabinti kwa ajili ya kupunguza ndoa na mimba za utotoni mkoani
Tabora.
Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ilijengwa katika miaka ya 1909 lakini
ilikuwa haina sehemu ya watu kukaa wakati wakisiburi kuona wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment