Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa huo amesimamisha kwa muda uchimbaji wa madini aina ya
dhahabu katika machimbo ya Kitunda wilayani Sikonge ili kuepusha maafa
zaidi yasije yakatokea.
Hatua hiyo
inafuatia maafa yaliyokea hivi karibuni ambapo wachimbaji wadogo wadogo
sita walifariki baada ya kufukiwa na kifusi na mmoja kufariki kwa kukosa
hewa wakati wa uchimbaji wa dhahabu katika eneo la Kitunda wilayani
Sikonge.
Uamuzi huo
umetolewa jana wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabaora Bw, Mwanri
baada ya yeye na kwa kushirikiana na Kamati na Ulinzi na Usalama mkoani
humo kutembelea machimbo yalisababisha maafa hayo kwa ajili ya kujionea
na kasha kuwapa pole wafiwa.
Alisema kuwa yeye na Kamati yake wameona ni vema
wasimamishe kwa muda ili taratibu zote za kuhakikisha usalama na zile
Baraza la Taifa la Mazingira za mpango wa ulinzi wa
mazingira(Environmental Protection Plan) zinafuatwa kabla ya kendelea na
shughuli za uchimbaji.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa lengo ni kutaka
Wachimbaji hao waendele kuchimba katika hali ya usalama bila kuharatisha
maisha yao na nguvu kazi ya Taifa.
Kufuatia
hatua hiyo , Bw. Mwanri aliwaagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya
Kati na Magharibi Salim Salim na Afisa Madini Mkazi wa Tabora Laurent
Mayala kuhakisha kuwa umbali kutoka shimo moja la uchimbaji hadi jingine
unazingati matakwa ya Sheria na Kanuni kuliko ilivyo sasa ambapo kutoka
shimo hadi shimo ni mita 3 hali ambayo ni hatari.
Aliongeza kuwa ni vema Ofisi hizo zikahakikisha kuwa
wanawapanga wachimbaji wadogo wadogo hao kulingana na matakwa ya
kisheria na sio kuwaacha wachimbo ovyo ovyo ambapo hivi sasa mashimo
yako karibu karibu sana na hivyo kuhatarisha maisha yao .
“Mimi siko
tayari kuona watu wengine zaidi wanafariki kwa sababu ya uchimbaji
usiozingatia matakwa ya kisheria na ambao hauna baraka za NEMC. Hivyo
kaeni chini na wamiliki wa mgodi muwapange vizuri kwa kuzingatia sheria
na bila upendeleo” aliagiza Mkuu huyo wa Mkoa.
“Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ilishaahidi kuwa
itawashika mkono wachimbaji wadogo wadogo , lakini ni vema tukahakikisha
kuwa Mpango wa Ulinzi wa Kimazingira umezingatiwa na kuwepo na wakaguzi
watakao hakikisha kuwa taratibu za umbalimbali toka shimo hadi shimo
umezingatiwa ili kulinda usalama wao kwanza ” anasititiza Mkuu wa Mko
huyo
Alisema kuwa kuwepo kwa madini ya dhahabu katika eneo la
Kitunda ni neema , lakini neema hiyo neema hiyo ni vema utafutaji wa
neema hiyo ukazingatia taratibu bila kusababisha maafa mengine kama
yaliyotokea wiki iliyopita ambapo watu watano walifia mgodini , mmoja
alifia hospitalini na mwingine alikufa kwa kosa hewa katika mgodi
mwingine.
Aidha ,Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Maafisa Madini
kuharikisha katika ufuatiliaji wa Kibali cha NEMC na kuandaa Mpango Kazi
wa Uchimbaji Mzuri na salama ili vijana wanaojihusisha na uchimbaji wa
madini katika eneo la Kitunda wasikae muda mrefu bila kuendelea na kazi
yao ya uchimbaji madini.
Alisema kuwa vijana hao hawana kazi nyingine
wanayotegemea kujiingizia kipato zaidi ya uchimbaji wa madini katika
eneo hilo , hivyo ni vema watendaji hao kwa kushirikiana na wamiliki wa
mgodi huo kuhakikisha mambo yafanyika haraka iwezekanavyo.
Aidha alitoa kwa wachimbaji madini hao kukikisha kuwa
sehemu ya mapato yao wayatumie katika kuboresha maisha yao na familia
zao kwa kujenga nyumba nzuri, kuvaa vizuri kula vizuri na kulipa kodi
zinatakiwa ili neema hiyo iwe na tija kwao.
Bw. Mwanri alisema kuwa haitakuwa na maana ya kuwepo kwa neema hiyo kama watapata fedha na kuendelea kuishi maisha duni .
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora Wilbroad
Mtafungwa ametoa onyo kwa baadhi ya vijana wanaendesha vitendo viovu
katika eneo hilo kama vile uvutaji bangi, uporoaji na ubakaji kwa
kisingizio cha uwepo wa madini ya dhahabu kuacha mara mmoja la sivyo
hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoani huo ili kuimarisha
ulinzi na kuhakikisha wachimbaji hao wanaendesha shughuli zao katika
mazingira rafiki, limeamua kufungua Kituo Kidogo katika eneo hilo.
Hatua hiyo inalenga kuwepo na ulinzi saa 24 siku zote
kwa ajili kuwa tayari wakati wote kukabiliana na uvunjivu na amani na
sheria ambao unaweza kujitokeza..
Aidha ,RPC huyo pia aliwaonya wachimbaji wadogo hao
kutoenda katika machimbo wakati wote wa zuio hadi hapo watakaporuhusiwa
la sivyo watakabiliana na Askari watakaokuwa wakilinda machimbo hayo
Katika hatu nyingine , Kamanda huyo ameowanya Polisi wote
watakaokuwa wakilinda eneo hilo kutojihusisha na uchimbaji madini
kwani kufanya hivyo kutawasababisha migogoro na wao wakuwa wamekiuka
kiapo chao.
Eneo la mchimbo ya Kitunda linawachimbaji zaidi ya 10,000 ambao wanaendesha shughuli hizo .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment