Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
26.4.2017
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora(RAS) Dkt. Thea Ntara amewataka Wachimbaji Wadogo
wadogo waliopo eneo la Kitunda wilayani Sikonge kuzingatia matumizi
mipira ya kufanyia mapenzi(condom) wanapoamua kufanya hivyo ili
kujikinga na maambukizi yanayowekusababishia kupata Virusi vya UKIMWI.
Hatua hiyo itasaidia waweze kuendelea kuwa na afya nzuri itakayowasaidia kuishi maisha mengi na kukatiza ndogo zao.
Dkt.
Ntara alitoa kauli hiyo jana wilayani Sikonge wakati akitoa pole
kuifuatia Maafa ya wachimbaji Saba wa madini katika eneo la Kitunda
ambapo sita walikufa kwa kufukiwa na kifusi na mmoja alikufa kwa kukosa
hewa.
Alisema
kuwa umati wa wachimbaji ulipo katika eneoi hilo ni zaidi ya elfu kumi,
hivyo ni vema wakatumia mipira kujikinga na UKIMWI wakati wakifanya
mapenzi ili uwepo dhahabu hapo usije ukasababisha tatizo lingine katika
jamii hiyo na ile inayowazunguka.
Dkt.
Ntara alisema kuwa wachimbaji wengi katika eneo hilo bado wanaumri
mdogo hivyo ni vema wakalinda afya zaidi ili wasiweze kutumbukia katika
matatizo yatakayokazi maisha yao na kupoteza nguvu kazi ya Taifa ambayo
bado inahitajika sana kwa maendeleo ya nchi hii.
Alisema
kuwa ni vema wakatumia fursa hiyo ya uwepo wa dhahabu katika eneo hilo
kwa kulinda na kuimarisha afya zao na sio kutumia fursa hiyo kutafuta
matatizo ambayo wanaweza kujikinga nayo au kuyaepuka.
Aidha
, Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwataka baadhi vijana wenye tabia za
kubaki kuachana na tabia hiyo bali wafuate taratibu za maridhiano zaidi
ili kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI.
Alisema kuwa mtu anayetumia nguvu mara nyingi akumbuki kujikinga jambo ambalo linaweza kumsababishia yeye au mwenzake matatizo.
Katika
hatua nyingine RAS huyo ameaagiza Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya
Wilaya Sikonge Daktari Mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha wanapeleka kwa
wingi mipira ya kiume ya kufanyia mapenzi katika eneo hilo la wachimbaji
madini wadogo ili kuwakinga na maambukizi mapya ya VVU.
Alisema
kuwa eneo lina wanchi wengi , hivyo ni vema wakapelekewa vifaa vya
kujilinda ili waendelee kuwa na afya bora ambazo zitawasaidia wao
kujitafutia kipato halali na kuchangia katika ujenzi wa nchi kwa njia
mbalimbali ikiwemo ulipaji wa kodi.
Dkt.
Ntara aliwaagiza pia viongozi hao kupeleka huduma mbalimbali kama vile
za kufungua Zahanati, Mtaalamu wa Afya, kufungua Shule ya Awali kwa
ajili kukabiliana na wingi wa watu katika eneo hilo ili nao kama walivyo
wananchi wapate fursa za huduma za jamii kwa karibu.
Alisema
kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi
wanaelimishwa juu ya kujilinda na magonjwa ya mlipuko kama vile
kipundupindu , na pia kuwapa matibabu pindi wanapokuwa na magonjwa
mbalimbali kama vile malaria.
Aidha
, Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwataka wachimbaji madini hao kuzingatia
usafi ili wasije wakapata maambukizi ya kipindupindu.
Alisema kuwa eneo hilo linawananchi wengine endapo usafi usipozingatiwa upo uwekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko.
Katika hatua nyingine
Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora amewataka vijana wote walipo
katika eneo ambao hawajafanya tohara kufanya hivyo ili kuimarisha afya
zao na kujikinga na magonjwa ambayo yanasababisha na wanaume kutofanya
hivyo.
Alisema kuwa huduma hizo zinatolewa katika Hospitali nyingi ni vema wakachangamkia fursa hiyo.
0 comments:
Post a Comment