Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
Serikali
ya Mkoa wa Tabora imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani
humo kuhakikisha zinatoa mikopo ya asilimia tano kwa vijana na wanawake
ili waweze kujiendeleza katika vikundi vyao na kuwa sehemu ya ajira.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati
wa kilele cha sherehe za Mei Mosi kwa ngazi ya Mkoa huo.
Alisema
kuwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote wanapaswa kuhakikisha
watoa asilimia hizo kwa wakundi hao mawili kupitia mapato yao ya ndani
kama sehemu ya kuyawezesha makundi hayo ili yaweze kutengeneza ajira na
kujiingizia kipato na kuondokana na umaskini.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema kuwa ajira ya Serikali pekee hazitoshi ni vema
wananchi nao wakijiari kupitia kujiunga katika vikundi vikundi na
kuanzisha mradi utakaotoa fursa ya ajira kwa watu wengi.
Aliagiza
Wakurugenzi wote Halmashauri kutoa mikopo ya asilimia tano ya mapato
yake ya ndani na kisha yeye apate taarifa za orodha na majina ya vikundi
na nakala ya kivuli cha hundi ya wanafuika.
Mkuu
Mkoa huyo aliongeza kuwa lengo la serikali ya Awamu ya tano ni
kuhakikisha kuwa wananachi wanawezeshwa na kuwekewa mazingira mazuri ya
kujiari wenyewe kupitia sekta mbalimbali.
Alisema
kuwa ili kuhakikisha kuwa vikundi vya kimama na vijana wanapata mikopo
ya asilimia tano ya fedha zinazotokana na mapato ya Halmashauri ya ndani
amewaagiza Mwenyeviti na Meya kusimamia utekelezaji wa agizo lake.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa Halmashauri zote za
Mkoa wa Tabora kuweka mazingira mazuri kwa wafanyakazi wapya au
wanaohamia ili wavutiwe na kufanyakazi katika mazingira yao.
Alisema kuwa waige
mfano wa Halmashauri nyingine hapa nchini ambazo zimekuwa na utaratibu
wa kuwanunulia thamani za ndani na runinga wafanyakazi wapya kama
kivutio kwao kupenda kufanyakazi katika maeneo yao mapya.
Bw. Mwanri alisema kuwa
wao wanaweza hata kuwaandalia nafaka kama vile mpunga , maharage na
nyumba nzuri ya kuishi ili asiwe kuwaza kuondoa au kuacha kazi kutokana
na mazingira magumu.
Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment