Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Serikali ya
Mkoa wa Tabora imewaagiza kwa wakazi wa Mkoa huo kuanza kulima kwa wingi
mazao wengine kama vile alizeti , pamba, mpunga na miembe ya kisasa
ili waweze kuwa na fursa pana ya kujiongezea kipato badala ya kutegemea
tumbakuli pekee kama zao kuu la uchumi katika maeneo mengi.
Kauli hiyo
imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati
anawahutubia wakazi na Wafanyakazi kwenye sherehe za kilele cha Mei Mosi
kilichofanyika katika Maspiaa ya Tabora.
Alisema kuwa
Mkoa huo umebahatika kuwa na ardhi ambayo mazao mbalimbali kama vile
mpunga , pamba, alizeti na hata matunda kama vile maembeo yanastawi ,
lakani bado wananchi hawayapa kipaumbele.
Bw. Alisema
kuwa wananchi wakiyapa kipaumbele na kwa kuzingatia ukulima wa kisasa
yatasaidia kufungua fursa ya uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo
kuelelekea viwanda vikubwa kwa kuwa malighafi itakuwepo ya kutosha
viwanda vitakavyoanzishwa.
Aliseme kuwa
endapo kila familia itakuwa walau na hekari moja ya shamba la alizeti
Mkoa wa Tabora utakuwa ndio mzalishaji mkubwa na mafuta hayo na
wawekezaji wengi watajitokeza kuanzisha viwanda wa usindikaji wa zao
hilo na hivyo kutoa ajira kwa wakazi wengi na wakinamama kupata fursa ya
kuuza vyakula.
Mkuu huyo wa
Mkoa aliongeza kuwa Tabora inayofursa kubwa ya kuwa na viwanda vikubwa
vya kusaga na kukoboa nafaka endapo wakulima watalima mpunga na mahindi
kwa wingi na kwa kuzingatia utaalam.
Kuhusu suala
la kilimo cha miembe, mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa wakazi wa
kuanza kuwa na mashamba makubwa ya miembe ya kisasa kwa ajili ya
kuongeza uzalishaji wa matunda hayo kwa ajili ya matumizi ya majumbani
na viwandani.
Alisema kuwa
Serikali ya Mkoa wa Tabora imeshaanza taratibu mbalimbali za
kuhakikisha kuwa viwanda vya zamani vinafufuliwa na vipya kama vile vya
kusindika tumbaku vinajengwa ili kuongeza ajira kwa wakazi wa Tabora.
Aidha alitoa
kwa wafanyakazi wote Mkoani humo kuonyesha mfano kwa kushiriki katika
shughuli mbalimbali za kilimo kwa kuwa na mashamba ya kisasa kama sehemu
ya kuhamasisha wananchi juu ya kilimo cha kisasa ambacho kinafaida
zaidi.
Maadhimisho ya Mei Mosi Kimkoa yamefanyika katika Manispaa ya Tabora ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni Uchumi wa Viwanda Uzingatie Haki , Masilahi na Hershima ya Wafanyakazi.
0 comments:
Post a Comment