Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri awaagiza wafanyabiashara wote walioko
katika eneo la machimbo ya dhahabu Kitunda wilayani Sikonge kuhakikisha
wanakuwa na maeneo ya kuhifadhi taka ngumu na laini kwa ajili ya
kujikinga na magonjwa mbalimbali hasa yale ya mlipuko.
Mkuu wa Mkoa
huyo alitoa agizo hilo jana wilayani humo wakati anaongea na wakazi wa
Kitunda wanajihusisha na uchimbaji wa dhahabu au utoaji wa huduma za
vinjwaji na chakula machimboni hapo.
Alisema kuwa
hakuna hatakayeruhusiwa kuendesha shughuli zake mbalimbali ziwe za
uchimbaji au biashara chakula na vinjwaji kama hatakuwa amechimba choo
na kuweka kifaa cha kutupa mabaki ya taka ngumu na laini.
Bw. Mwanri
aliongeza kuwa eneo hilo linahitaji usafi wa hali ya juu kwa sababu ya
idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambapo inaweza
kusababisha maafa itatokea mtu mmoja akaugua ugonjwa wa mlipuko kama
vile kipindupindu aliweza kuwaathiri watu wengi na wakati mwingine
kusababisha maafa ambayo yanaweza kuzuilika.
"Hapa lazima
tuhakikishe usafiri wa hali ya juu kwani tusipofanya hivyo tunaweza
kufa kama kuku waliougua ugonjwa wa kideli ...uongozi huu hako tayari
kuona mtu anafanyabiashara katika mazingira hatarishi kwa wateja
wake"alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha , Mkuu
huyo wa Mkoa aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge
kuleta Pipa kubwa la kutupa taka ili kulinda mazingira ya eneo hilo.
Kwa upande
wa wachimbaji wa eneo hilo amewaagiza kujiwekea taratibu za kutozana
faini kwa watu wanachafua mazingira kwa ajili ya kuhakikisha afya
zinaendelea kuwa salama na magonjwa ya mlipuko na hivyo kuendelea na
shughui za uchimbaji madini pindi watakaporuhusiwa.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment