Na Tiganya Vincent
Tabora
Uongozi wa
Mkoa wa Tabora umeamua kuendesha zoezi la kudumu la kuhamasisha jamii
kuanzia ngazi za wanafunzi hadi jamii nzima juu ya zoezi upandaji miti
ili kukabiliana na uharibifu mkubwa wa mazingira ulisababishwa na
shughuli mbalimbali za kibinadamu mkoani humo.
Hatua
hiyo inalenga kuijengea jamii na wanafunzi katika shule na vyuo tabia
ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti kwa ajili ya faida yao na
kizazi kijacho.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey
Mwanri wakati akiongoza zoezi la upandaji wa miti zaidi ya 150 katika
eneo la Malolo barabara ya zamani ya kutoka Tabora mjini kuelekea
Urambo.
Alisema
kuwa zoezi hili ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Makamu wa
Rais ambapo kwa kuanzia amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri zaote kuhakikisha kila Wilaya inatekeleza agizo
hilo kwa miti isiyopungua milioni moja na laki tano kila mwaka.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliongeza kuwa miti waliyopanda watakikisha inahimili
wakati wa kiangazi kwa kuimwagilia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya
umwagiaji kwa matone ya chupa.
Alizitaja
baadhi ya sababu zilizosababisha kuwepo ya uharibifu huo mkubwa ni
pamoja kilimo cha tumbaku, ulimaji katika vyanzo vya maji na ufugaji
usio rafiki wa mazingirana.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa hatua nyingine ambazo zimeanza kuchukuliwa katika
kudhibiti uharibifu wa mazingira hasa maeneo ya mijini ni pamoja na
kukamata mifugo yote inayozurura.
Aidha , aliwashukuru wanyakazi wa NBC tawi la Tabora kupanda miti hiyo na kuahidi kuitunza ili ije iwe ukumbusoa wao wa kufanyakazi katika Mkoa huo.
Bw.
Mwanri alisema kuwa kitendo chao cha upandaji wa miti katika Mkoa huo
sio tu kwamba watakuwa wanahifadhi mazingira bali watabakiza alama
ambayo itakuwa ukumbusho kwao na kwa kizazi chao.
Kwa
upande wa Meneja wa NBC wa Kanda (Tabora, Shinyanga, Kigoma na Mara)
Daudi Edgar Mfalla alisema kuwa Benki hiyo imefurahishwa na juhudi za
Uongozi wa Mkoa huo na kuamua kuunga mkono zoezi linaloendelea kwa
sababu ya kutambua bila mazingira mazuri hakuna uhai.
Alisema kuwa upandaji wa miti hiyo ni sehemu ya utaratibu wa Benki hiyo wa kurudisha inachokipata katika jamii.
Bw.Mfalla
alisema kuwa zoezi linaloendwa na uongozi wa Mkoa wa Tabora ni zuri na
litasaidia kuijenga jamii hasa kuanzia watoto hadi wazee kuwa na mazoea
ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa ya faida yao , jamii,
Taifa na dunia kwa ujumla.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Benki hiyo mkoani Tabora Bibi Grace Mwanri alitoa
wito wa kujenga tabia ya kupanda miti na kuitunza kwani inahusika sana
na uhai na maisha ya kila ya mwanadamu.
Alisema kuwa jamii kama itakata miti ovyo bila kupanda mingine kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vyanzo itasababisha ukame na hivyo hakutakuwepo na maji na uhai utakuwa shakani.
Bibi
Mwanri alisema kuwa wao kama wafanyakazi na wakazi wa Tabora
wanalitambu hilo na ndio maana wameungana na viongozi na wadau wote
ambao wamekwishapanda miti kushiriki zoezi hilo.
Mkoa wa Tabora kabla ya uharibifu
wa mazingira ulikuwa ukipata mvua za wastani wa milimita 1800 lakini
kutokana na uharibifu huo hivi unapata wastani wa milimita 650.
0 comments:
Post a Comment