Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amewataka Wakurugenzi Watendaji
wa Halmashauri zote mkoani humo kuwashirikisha Wakaguzi wa Ndani na
Maafisa wa Ugavi na Ununuzi wakati wa ukaguzi miradi mbalimbali katika
maeneo yao ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora na inalingana na
thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Dkt.
Ntara ametoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati anafunga mafunzo ya
siku tano ya Wakaguzi wa Ndani wa Halmashauri zote ya Mkoa wa Tabora
yaliyohusu mbinu mpya za ukaguzi wa hesabu kufuatia mabadiliko katika
ukusanyaji wa mapato na maduhuli ya Serikali kuendeshwa kwa njia ya
mtandao.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kwa Halmashauri kutopokea miradi
iliyotekelezwa chini ya kiwango na hivyo kuiepusha Serikali hasara na
kutowakatisha wananchi wanakuwa wanaotarajia mradi uwasaidie.
“Nawagiza
Wakurugenzi katika Halmashauri zote nane za Tabora kuhakikisha
wanaongozana na Wakaguzi wa Ndani na Maafisa wa manunuzi ili waweze
kujiridhisha kama miradi inatekelezwa inalinga na fedha iliyotolewa na
hakuna udanganyifu wowote uliofanyika” alisisitiza Dkt. Ntara.
Aidha
Dkt. Ntara alitoa kwa Wakaguzi hao wa Ndani waliopata mafunzo hayo na
mbinu hizo za kisasa walizofundishwa kufanya kazi kwa ufanisi na
kuzisaidia Halmashauri kudhibiti upotevu wa fedha za Serikali katika
Halmashauri zao katika makusanyo ya maduhuli na miradi mbalimbali
inayotekelezwa katika maeneo yao.
Alisema
kuwa mafunzo waliyopata hatakuwa na maana kama hawatasaidia Halmashauri
zao katika kudhibiti matumizi mabaya ya maduhuli ya Serikali na hivyo
ni vema wakawa wa kwanza kuonyesha udhaifu ili hatimaye yafanyike
maboresho.
Mafunzo
hayo yaliwashirikishi wa washiriki 15 kutoka Halmashauri zote za Tabora
na yalitolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Idara ya Mkaguzi
Mkuu wa Ndani wa Serikali(IAG) ili kuwajengea uwezo na kuongeza tija
katika utendaji wa kazi za kiukaguzi.
Katika
mafunzo hayo washiriki walipata mafunzo ya matumizi ya komputya kwa
kutumia mbinu za kisasa za ukaguzi kufuatia maduhuli kilipwa kwa njia ya
kimtandao.
0 comments:
Post a Comment