RC TABORA AWATAKA VIJANA KUMCHAMUNGU
Na Tiganya Vincent,Sikonge .
Vijana
wametakiwa kumucha Mungu kwa kuwasikiliza na kutii maelekezo yanayotewa
na viongozi mbalimbali ikiwemo vingozi wa dini ili kujenga jamii yenye
maadili mema na yenye hofu ya kufanya mambo ambayo ni kinyume maagizo ya
Muumba wa Mbingu na Nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa
mkutano wa hadhara na Wachimbaji wadogo wadogo na kwenye maeneo
mbalimbali wilayani Sikonge.
Alisema sio vema wakachukua maneno ya vijiweni na
kufanya kama ndio msingi au mwongozo wa maisha yao ya kila siku, jambo
ambalo linaweza kuwasababisha wao kuijiingiza katika maovu ikiwemo
kudhani utajiri unapatikana na njia ya umwagaji damu ya watu wengine.
Bw.
Mwanri alisema kuwa utajiri unapatikana kwa mtu kufanyakazi kwa bidii
na kwa kumtanguliza Mwenyeji Mungu katika kila kazi halali anayoifanya.
Aliongeza
kuwa Serikali haina dini lakini inatambua kuwa wananchi wake wanadini
zao na ndio maana kila kwenye mkusanyiko au makazi ya watu inasisitiza yatengwe maeneo ambayo zitajengwa nyumba za Ibada ili Watanzania waweze kupata huduma hiyo muhimu.
Bw.
Mwanri aliwaonya vijana na baadhi ya watu wengine wasiendekeza maneno
ya vijiweni ambayo yanaweza kuwajengea fikira potofu za kudhani
mafanikio katika maisha yapatikana kirahisi na hivyo wengine kushinda
wakicheza drafuti, bao , Pool badala ya kufanyakazi.
Alisisitiza
kuwa vijana wanaoamini maneno potofu ya vijiweni ndio uweza hata
kudharau wakubwa na kuwaona kuwa wao wako juu yao na wakati mwingine
kufikiria kwenda Ulaya wakati hata nauli ya kufika kule hawana.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa njia pekee na bora ya kuwasaidia ni kuwatii
viongozi wote wa dini na jamii ndio utakuwa mwongozo mzuri wa kuwapeleka
tika mafanikio ya kweli.
Mkuu
huyo Mkoa yuko alikuwa katika ziara ya uhamasishaji na uelimishaji
makazi wa Sikonge juu ya zoezi la upandaji miti na pia kujionea shughuli
za uchimbaji wa madini katika eneo la Kitunda.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment