Na Tiganya Vincent, Sikonge
Serikali
ya Mkoa wa Tabora imesema mkazi wake anayepinga zoezi la upandaji miti
katika maeneo yake ni vema akatafuta sehemu nyingine ambayo hawako
tayari kuhifadhi mazingira.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Bw. Aggrey Mwanri wakati wa Mkutano wa
hadhara wilayani Sikonge alipokuwa akiwaelimisha juu ya zoezi
linaloendelea mkoani humo la kupanda miti ili kukabiliana na uharibifu
wa mistu uliosababishwa na shughuli mbali za binadamu.
Alisema
kuwa Mkoa wa Tabora unanyewelewa kugeuka kuwa Jangwa kama juhudi
zisipofanyika mapema kutokana na ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya
nishati ya kukaushia tumbaku , matumizi ya majumbani, ujenzi na ufugaji
wa kuhama hama ambao hauzingatia utunzaji bora wa mazingira.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa mtu au kikundi chochote kitakachokaidi zoezi hilo
la kukarabati upya uoto wa asili na upandaji wa miti katika Mkoa wa
Tabora , kitakuwa hakiwataki mema wananchi .
Alisisitiza
uharibifu uliofanyika umesabibisha upungufu mkubwa wa mvua katika mkoa
huu na kufanya vyanzo vingi vya maji kukauka na hivyo kuhatarisha maisha
ya wakazi wake.
Mkuu huyo Mkoa alisema suala la kupanda miti ni la wakazi wote wa Tabora na sio la viongozi wa Serikali, mashirika ya umma , wanafunzi na dini pekee.
Aliongeza
kuwa kipindi hiki ndio kizuri cha kupanda miti kwani ikimwagiliwa
vizuri kwa kutumia teknolojia ya matone na wakati ikigonja mvua
haitakufa.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw.
Simon Ngatunga alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Tabora ,kuwa wao
wamenunua miti maji 5078 na kilo 38 za miti kutoka mkoani Dodoma kwa
lengo la kupanda na kuzalisha miche zaidi 10,000 ili kuendeleza zoezi
hilo la upandaji miti.
Alisema
kuwa lengo ni kuhakikisha mitaa yote ya Halmashauri ya Wilaya hiyo
inakuwa na miti kwa ajili ya kuupamba mji wa Sikonge na utunzaji wa
mazingira.
Bw.
Ngatunga alitoa wito kwa wananchi ambao miti imepandwa katika maeneo ya
shughuli zao mbalimbali ikiwemo biashara kuhakikisha wanaitunza miti
hiyo kwa kuimwagiliaji ili isije ikafa.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment