Daktari Bingwa kutoka China akipokea mkono wa asante kutoka kwa Naibu
Waziri wa Afya
Madaktari bingwa kutoka China wakifuatilia ufunguzi huo
Dk.Kigwangalla akimuongoza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri amezindua rasmi kambi maalum ya
huduma za Afya juu ya upimaji wa Afya bure kwa wananchi mbalimbali
Wilayani Nzega, ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanri ambaye alikuwa mgeni
rasmi, aliwapongeza waandaaji wa kambi hiyo kwani itasaidia kuboresha
afya za wananchi ili kuwa na afya njema.
“Wananchi wanahitaji
Afya njema, tunapongeza kwa kambi hii kwani madaktari bingwa waliokuja
hapa watatua matatizo ya msingi kwenye afya zetu. Hivyo wananchi
mujitokeze kwa wingi” aleleza RC Mwanri.
Aidha, Mh. Mwanri
amewapongeza Madaktari bingwa kutoka China ambao wanaendesha kambi hiyo
ya siku Sita, iliyoanza rasmi Julai 24 na inatarajia kumalizika Julai
30.
Hata hivyo, Mh. Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wote wa Mkoa wa
Tabora waupokee mpango huo wa kambi za huduma za Afya ili uende mkoa
mzima kwani wanakosa fursa ya kuonana na Madaktari bingwa.
“Ni
jambo zuri, tunaomba Wakurugenzi wote mulipokee suala ili wa Mkoa wa
Tabora ili liendelee Mkoa mzima. Pia ni wasaha kwa wananchi wote kupeana
taarifa ili zienee kwa watu wote wajitokeze hapa Nzega kupatiwa huduma
za upimaji na matibabu.” Alieleza Mh. Mwanri huku akimuagiza Mganga Mkuu
ahakikishe anaratibu mpango huo uenee Mkoa nzima wa Tabora.
Kwa
upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega
Vijijini ameshukuru Serikali ya China kwa kufanikisha tukio hilo ikiwemo
kutoa dawa za Maralia kwani kwa msingi huo utasaidia kuokoa maisha ya
wananchi wa Nzega.
“Tunapokea kwa mikono miwili msaada huu wa
kutoka Serikali ya China hasa kupitia kwa Balozi wake hapa nchini
Tanzania. Dawa hizi ni nyingi nahakika zitasaidia wananchi wote kuanzia
wilaya ya Nzega na Mkoa nzima wa Tabora kwa ujumla. Nawashukuru sana
wananchi wanaojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuja kupata huduma za
matibabu kwenye kambi hii ya madaktari bingwa hapa Nzega” alieleza Dak.
Kigwangalla.
Zoezi hilo la Upimajj wa Afya Bure Wilayani Nzega,
limeandaliwa na Wabunge wa majimbo yote ya Nzega ambapo imeanza kuanzia
hiyo Julai 24 na itatarajiakumalizika Julai 30, huku kwa wakazi wote wa
Nzega na jirani wata pima afya zao bure na kupata huduma za matibabu
bure, ikiwemo upasuaji.
Tayari timu ya Madaktari bingwa wa kila fani ya tiba wapo kwenye kambi hiyo inayoendelea kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nzega.
0 comments:
Post a Comment