Mkuu
wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri, akizungumza na maofisa ugani wa
wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa hayo
yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB),
wilayani humo mkoani Tabora leo. Kutoka kushoto ni Mtafiti Bestina
Daniel kutoka COSTECH, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo,
Hashim Kazoka na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pascal Ngunda.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pascal Ngunda, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Costech.
Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Renatus Mahimbali akizungumza.
Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia, Dk.Nicholaus Nyange akitoa mada kwa maofisa ugani hao.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Hashim Kazoka, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akizungumza. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya, Emanuel Alex.
Mshauri
wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia, Dk.Nicholaus Nyange (kulia),
akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa
wilaya hiyo, Peres Magiri wa tatu kulia.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Maofisa ugani.
Mafunzo yakiendelea.
Watoa mada wakisubiri kuwajibika. Kutoka kushoto ni Mshauri
wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia, Dk.Nicholaus Nyange, Mtafiti wa
Mazao ya Kilimo kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru mkoani
Mwanza, Bakar Japhet, Mtafiti wa zao la pamba kutoka Ukiriguru Stellah
Chilimi na Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Dotto Mwaibale, Sikonge-Tabora
VIONGOZI
wa Halmashauri wametakiwa kuacha kuwapa kazi za kiutendaji maofisa
ugani badala yake wametakiwa kuachwa waendelee na shughuli zao za ugani
ili kuinua kilimo.
Mwito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter
Nzalalila wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani
wa wilaya hiyo mkoani Tabora leo asubuhi.
"Napenda
kuwaeleza viongozi wa halmshauri wawaache maofisa ugani wafanye
shughuli zao za ugani badala ya kuwapa kazi za utendaji ambazo zinapaswa
kufanya na maofisa watendaji wa kata na vijiji" alisema Nzalalila.
Alisema ili kilimo kiweze kusonga mbele ni lazima wataalamu wa kilimo wakabaki katika kazi yao na si kufanya kazi za watendaji.
Nzalalila
aliwataka maofisa ugani hao kila mmmoja kuwa na mpango wa kujua idadi
ya wakulima katika eneo lake la kazi pamoja na mahitaji yao kama
pembejeo ikiwemo mbolea ili iwe rahisi kujua mahitaji ya wakulima.
Alisema
Mkoa wao umepata bahati ya pekee kwa wataalamu wake kupata mafunzo hayo
ambayo yanalenga kuwaongezea ujuzi na kuwakumbusha majukumu yao.
Alisema
wilaya inaamini mafunzo hayo yatasaidia kuinua kilimo cha kisasa katika
wilaya hiyo na kuongeza uzalishaji wa mazo ya chakula kama mahindi,
mihogo na mpunga.
Alisema
mazao yote matatu ya chakula ya Mahindi,Mihogo na mpunga ni mazao
muhimu kwa chakula kwa wakazi wa wilaya hiyo hivyo mafunzo hayo yawe
chachu mpya katika kufanya mapinduzi kwenye kilimo na kuwataka kutumia
mbinu hizo kuzalisha zao la biashara la Tumbaku kitaalmu kuwaandaa
wakulima na mpango wa serikali ya viwada.
Akizungumza
wakati akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya hiyo Peres Magiri aliagiza
pembejeo za Kilimo zikifikishwe kwa wakati kwa wakulima kabla ya kuanza
mimu wa kilimo ili wakulima waweze kupata muda wa kuandaa mashamba yao.
Alisema
iwapo pembejeo za kilimo zikimfikia mkulima kwa wakati itamsaidia
kujiandaa vizuri kuliko kumcheleweshea jambo ambalo linamrudisha nyuma
katika kilimo.
Magiri
aliwataka maofisa ugani hao kupokea mafunzo na kuyapeleka wa wakulima
ili kuwasaidia kupata mbinu mpya za uzalishaji na zinazotumia teknolojia
za kisasa katika kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao mbalimbali
yanayolimwa kwenye maeneo yao.
Mtafiti
Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Costech alisema mafunzo
hayo yameandaliwa na Costech kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa
maendeleo ya kilimo nchini (OFAB)
“Tumeona
tuendeshe mafunzo haya kwenu ili kuwakumbusha majukumu yenu na
kuwapatia mbinu mbalimbali ili muweze kutekeleza majukumu yenu vizuri
maana wakulima wanawategemea nyinyi kuwasaidia kupitia taaluma yenu
hiyo” alisema Daniel Daniel.
Alisema
ili mafunzo hayo yaweze kuleta maana kwa wakulima na Serikali hawana
budi kuyafanyia kazi kwa kwenda kuwafundisha wakulima kwa vitendo mbinu
hizo za uzalishaji kwa kuanzisha mashamba madogomadogo ili wakulima
waweze kuona na kisha nao kufuata kwa vitendo mbinu hizo pale
watakapoona matokeo mazuri kwenye mashamba yao ya mfano.
Mafunzo
hayo baada ya kumalizika kwenye wilaya za mkoa wa Geita sasa
yanaendelea kwenye Mkoa wa Tabora na wilaya zake ambapo mpaka sasa
tayari yameshafanyika kwenye wilaya za Igunga,Nzega, Uyui, Sikonge na
kesho yataendelea kwenye wilaya za Urambo.
0 comments:
Post a Comment