Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Ileje baada
ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya hiyo akiwa katika ziara ya
mkoa wa Songwe Julai 22, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge Janet Mbene wa Ileje
(kulia) na Juliana Shonza wa Viti Maalum baada ya kuwasili kwenye makazi
ya Mkuu wa wilaya ya Ileje kuanza ziara wialyani humo Februari 22,
2017. (Picha na ofisi ya Wziri Mkuu).
Baadhi
ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na taasisi binafsi wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Ileje
Julai 22, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma, viongozi wa
dini na viongozi wa taasisi binafsi mjini Ileje Julai 22, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la hospitali ya wilaya
ya Ileje akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe, Julai 22, 2017. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto) wakitazama mbegu za
mahindi zinazozalishwa na Kikundi cha SAM cha Ileje wakati alipotembelea
banda la kikundi hicho kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye
stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaranga wa samaki wakati
alipotembelea banda la Kikundi cha wanawake cha Tukazane cha Ileje
kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje
Julai 22, 2017.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 1.669 kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya ya Ileje mkoani
Songwe.
Ametoa
kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 22, 2017) wakati akizungumza na
watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje katika ukumbi wa Shule ya
Sekondari Itumba.
Waziri
Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. bilioni moja zimetengwa kwa ajili
ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji miwili ya Isongole na Itumba
wilayani Ileje.“Kiasi kingine cha sh. milioni 669 kimetengwa kwa ajili
ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ileje katika mwaka wa
fedha wa 2017/2018.
Hata
hivyo, amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa Kampeni ya Rais
Dkt. Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji
kwa urahisi.Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha
wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na
salama katika umbali usiozidi mita 400.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Songwe kuhakikisha inaimarisha ulinzi katika maeneo ya mipaka.Amesema
kamati hiyo inatakiwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka ili
kuizua wageni kuingia bila ya kufuata taratibu zilizowekwa kisheria.
Awali
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Bw. Joseph Mkude alisema katika kipindi cha
Julai 2016 hadi Juni 2017 jumla ya wahamiaji haramu 38 walikamatwa
kwenye wilaya hiyo.Alisema kati ya wahamiaji hao haramu 36 ni raia wa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wawili walikua raia wa Malawi
na wote walirudishwa makwao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 22, 2017.
0 comments:
Post a Comment