Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameagiza kuanzia msimu ujao
wa kilimo kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi ni lazima alime heka
mbili za alizeti kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kujenga Viwanda vya
kusindika na kuzalisha mafuta hayo kuanza ujenzi mkoani humo.
Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane
kwa Kanda ya mikoa ya Magharibi yaliyofanyika mkoani Tabora.
Alisema zao la alizeti katika mkoani Tabora
linastawi sana
na ikiwa wakazi wake watalima kwa wingi Kampuni mbalimbali zitajitokeza
kwa wingi kuja kujenga viwanda vya kuzalisha mafuta hayo.
Bw.Mwanri
alisisitiza kuwa wawekezaji wengi wamekuwa wanashindwa kuja kujenga
viwanda vya usindikaji wa mafuta
hayo kwa sababu siku za nyuma zao hilo limekuwa halitiliwi mkazo na
kufanya uzalishaji kuwa wa chini sana , lakini hivi sasa hiyo itakuwa
ajenda ya Mkoa kama mkakati mojawapo wa kuwavutia watu kuja kujenga
viwanda.
“Ndugu zangu Wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi kuanzia sasa akili yetu na agenda yetu kubwa iko
katika kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Tabora analima heka
mbili za alizeti kuanzia msimu ujao wa kilimo ili tuwe na malighafi
nyingi kwa ajili ya kulisha viwanda vitakavyoanzishwa kwa mwaka mzima”
alisema
Mkuu huyo Mkoa.
Katika kutekeleza agizo hilo aliwaagiza Maafisa Ugani wote mkoani hapa kuhakikisha wanawatembelea wakulima vijijini
kwa ajili ya kuwaelimisha juu ulimaji bora na mbegu bora za zao hilo kwa ajili kuwafanya wakulima kuanza mara moja kilimo hicho pindi mvua za masika zitakapoanza.
Katika
hatua nyingine aliwaagiza Wakurugenzi Watendaji wote na Maofisa Ugani
wote kuhakikisha kuwa wanaanza wanawahimiza
wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa huo kuanza kilimo cha zao la uwele ,
mtama, viazi na mihogo ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula
kwa sababu ya mvua kuendelea kunyesha chini ya kiwango.
Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuendelea kung’ang’ania mazao yanatumia miezi mingi kukomaa kusababisha wakazi
hao kuendelea kukabiliwa na upungufu wa chakula wakati wakilima mazao yanayostahimili ukame tatizo haliwezi kuwapata.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nzega alisema kuwa wao tayari wameshaanza maandalizi kwa kuwa na shamba la mfano la heka
10 ambapo tayari wameshazalisha alizeti na kutoa mafuta.
Alisema
kinachofuata ni kuongeza wigo wa kilimo hicho wa kuwashirikisha
wananachi wengi kwa kuwaelimisha juu ya
kilimo bora cha zao hilo ili waweze kuzalisha kwa wingi na kutoa fursa
kwa wamiliki wa viwanda kupata malighafi ya kutoa kwa ajili ya
uzalishaji mafuta.
Naye Mkazi wa Ipuli mkoani Tabora Juma Elia aliunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora la kuhamasisha
wakulima kuanza kulima alizeti ambalo ni rafiki na mazingira kwa sababu halihitaji kuni kukauka kama ilivyo tumbaku.
Aliongeza kuwa zao hilo litasaidia kutoa ajira kwa njia ya vijana kushiriki kilimo na wengine kuajiriwa katika
viwanda vya kusindika mafuta ya alizeti vitakavyoanzishwa.
0 comments:
Post a Comment