Home » » MWALIMU KORTINI KWA MAPENZI NA MWANAFUNZI

MWALIMU KORTINI KWA MAPENZI NA MWANAFUNZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Imeandikwa na Lucas Raphael, Igunga
MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35) amefi kishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya mapenzi na mwanafunzi wa mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa). Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa