Na  Bashir  Yakub.
Maudhui  katika  makala  haya yanatoka  katika  Sheria  ya  Ndoa, sura  ya  29, iliyofanyiwa  marekebisho  2010,  pamoja na  Sheria  ya Usimamizi  na  Uendeshaji  wa  Mirathi,Sura  ya  325,  R;E 2002.  Ziko  aina  mbili  za  mali  anazostahili  mjane.
 Kwanza  ni  mali  inayotokana  na  machumo  ya  pamoja  yeye  na  marehemu  mme  wake .  Pili  ni  urithi  anaostashili  kupata   kama  mrithi  wa  marehemu.
Kwa  mfano,  mume amefariki. Lakini  kabla  hajafa   huko  nyuma  walijenga  nyumba  yeye  pamoja  na  mke  wake. Au  walinunua  kiwanja  yeye  na  mke  au  gari  nk. Mme  sasa  amefariki   na kuacha  hizo  mali.   Katika mali  ya  namna hii  kuna  sura  mbili.
Sura  ya  kwanza ni  kuwa  katika  mali  hii  kuna  “share” ya  mme  na  kuna  “share  “  ya  mke.  Na  “share”  ya  kila  mmoja  inatokana  na  ukweli  kuwa  kila mmoja  kati  yao  alichangia  kupatikana kwa  hiyo  mali. Kwahiyo  kila  mmoja  ana “share”  yake  kutokana  na kile  kiwango alichochangia.  Na  mchango tulishasema  kuwa sio  leta  ni  lete. Hata  kazi  za  nyumbani kama kupika, kufua, kulea  watoto  nk. nazo ni  mchango katka kupatikana  kwa  mali.
Sura  ya  pili, ni  kuwa  kama  mume  amekufa basi  mwanamke  kama  mke  halali  anastahili  urithi  kutoka  mali  za  mumewe. Urithi  huu  utatoka  katika  zile  mali  anazomiliki  mumewe  yeye  kama  yeye. Urithi utatoka  katika “share”  ya mume  na  si  katika “share”  nyingine.
Kwahiyo  katika  mali  ileile  mjane  atakuwa  na  haki  za  aina  mbili.  Haki   ya  kupata  sehemu  yake  aliyochangia  katika  kupatikana  kwa  mali,  na  haki  ya kurithi   mali  ya  mme  wake.
KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment