Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia
Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena
Mtenga wakiangalia mashine ya kuingia shimoni inayotumiwa na Wachimbaji
wadogo wa mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani
Tabora.
Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia
Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena
Mtenga wakionyeshwa na Afisa madini kanda ya Taabora Injinia Kasweke
aina za mawe yenye dhahabu yanayopatikana katika Mgodi mdogo wa Igulubi
wilayani Igunga mkoa wa Tabora.
Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia
Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena
Mtenga na Afisa Mazingira Bi Suzan Nchala wakiangalia sehemu ambapo mawe
yaliyopondwa husafishwa ili kupata dhahabu walipotembelea mgodi wa
Igulubi wilayani Tabora.
Mmiliki wa mgodi mdogo wa Igulubi Bwana Steven Siyame akiwaonyesha
wajumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais waliofanya ziara katika mgodi huo
uliopo Igunga Tabora jinsi mashine ya kuvunjia mawe inavyofanya kazi(
haipo pichani)
Wachimbaji wadogo wa migodi wametakiwa kutunza mazingira katika maeneo
yote yanayozunguka migodi pamoja na usalama kwa Wafanyakazi katika
katika migodi hiyo. Rai hiyo imetolewa na ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu
wa Rais ulipotembelea mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga
mkoani Tabora katika ziara inayofanywa na Ujumbe huo wa kutembelea
migodi ya Wachimbaji wadogo.
Wakiongea katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Bi Magadalena Mtenga walisema kuwa utunzaji wa mazingira ni kitu cha muhimu sana na pia usalama kwa Wafanayakazi katika migodi hiyo ni muhimu pia. Walimshauri Mkurugenzi wa mgodi huo Bwana Steven Siame kuwa karibu na Taasisi za Serikali ili kuweza kufahamu mambo yote yanayotakiwa katika suala zima la uchimbaji ikiwemo Baraza la Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya kujua kanuni za utunzaji wa mazingira.
Ujumbe huo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais upo katika ziara ya kutembelea migodi midogo inayomilikiwa na Wachimbaji wadogo kwa ajili ya kujifunza na kuona shughuli hizo za Uchimbaji zinavyofanyika katika migodi hiyo likiwemo na suala la utunzaji wa Mazingira kwa ujumla.

0 comments:
Post a Comment