NA TIGANYA VINCE.
25 September - 2017.
RS-TABORA.
WATU
wawili wanasadikiwa kujihusisha vitendo vya wizi wa pikipiki wamefariki
dunia hapo hapo baada ya kupigwa na kuchomwa moto wananchi wenye hasira
kali wakati wakijaribu kumyang’anya pikipiki dereva wa bodaboda majira
ya saa nne usiku.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora
Wilbrod Mutafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema
kuwa hatua hiyo ilitokana na watu hao ambao hadi hivi sasa majina yao
hajajulikani kumukodisha na kisha kumteka dereva bodaboda na walipofika
eneo la Malolo lililopo Manispaa ya Tabora walianza kumchoma kisu kwenye
shavu la kushoto kwa nia ya kutaka kumpora pikipiki.
Mutafungwa
alisema kuwa baada ya Dereva wa Bodaboda kuchomwa kisu alipiga kelele
za kuomba msaada na wananchi walijitokeza , baada ya wezi kuona watu
wanakuja walijaribu kukimbia lakini hawakufanikiwa kufika mbali na ndipo
walikamatwa na kuanza kupigwa hadi walipofariki.
Alitoa
wito kwa watu ambao ndugu zao hawaonekani kufika Hospitali ya Mkoa wa
Tabora Kitete kuwatambua watu hao ambao majina hayo haya fahamiki.
Kamanda
Mutafungwa alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo ili kubaini majina ya watu hao na watu ambao wamekuwa
wakishiriana nao katika vitendo vya kihalifu ikiwemo utekaji wa Boda
boda.
Aliongeza
kuwa wanaendelea na uchunguzi wa watu waliohusika katika kujichukulia
Sheria mkononi ili waweze kufikishwa katika vyombo vya maamuzi.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Manispaa ya Tabora Waziri
Kipuzi aliwataka madereva kuwa makini na watu wanawakodisha nyakati za
usiku kwani wapo ambao wana nia mbaya.
Katika
hatua nyingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroard Mtafungwa
alisema kuwa hadi hivi Jeshi hilo linawashikilia watu 54 kwa tuhuma za
kuhusika na tukio la kuwapiga na kuwachoma moto katika sehemu zao za
siri wanawake wanne katika kata ya Loya wilaya ya Uyui.
0 comments:
Post a Comment