NA TIGANYA VINCENT
2 NOVEMBA 2017
KUCHELEWA
kupelekwa fedha ambazo zilitakiwa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
wananchi ili waweze kukamilisha Mradi wao wa Ujenzi wa jengo la Mashine
ya Usindikaji wa Mafuta katika Kijiji cha Kombe umesababisha Mwekahazina
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kupewa wiki mbili kuhakikisha fedha
hizo zinafika haraka la sivyo atakuwa amejiundoa kazini mwenyewe.
Msimamo
huo umetolewa jana wilayani Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Mashine ya
kukamulia mafuata ya alizeti ambao umekwama kumalizika kwa zaidi ya
miezi mitatu baada ya Halmashauri kuchelewa kupeleka fedha ambazo
ilitakiwa itoe.
Alisema
kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wananchi wamejituma kujenga jengo
kwa ajili ya kuweka mashine ya kusindika mafuta ya alizeti lakini
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua hadi hivi sasa hajitoa milioni 4
zilizotakiwa kuunga mkono nguvu za wananchi hao.
Aidha
Mwanri aliongeza kuwa pia kiasi kingine ni zile milioni 17 zilizotolewa
na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Miombo kwa ajili shughuli mbalimbali
kama vile ufugaji kuku, kilimo cha uyoga, ufugaji nyuki zimekwama
kupelekwa kwa walengwa kwa sababu ya Ofisi ya Uhasibu ya Halmashauri
hiyo kuchelewesha wakati Wilaya nyingine zimeshapeleka kwa walengwa na
kuanza kufanyakazi.
Alisema
kuwa hawezi kumvumilia mtumishi wa sampuni hiyo ambaye ameshindwa wa
kutumia fedha miradi kwa wakati ambazo zimetengwa kwa ajili ya
kuwasaidia wananchi katika kuwainua kiuchumi na kuwaletea maendeleo yao
na taifa kwa ujumla kwa sababu ya urasimu usio na maana kwani kufanya
hivyo ni kuwakatisha tamaa.
Mwanri
alisema kuwa ndani ya wiki mbili mbili anataka kupata majibu ya hatua
ambazo zimefikiwa katika kuhakikisha kuwa fedha hizo za mradi endelevu
wa miombo zimeshapelekwa eneo husika na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
imeshawakabidhi wananchi hao milioni 4 ili wamalizie jengo la mashine
yao.
Mwanri alisema kuwa kinyume cha hapo wahusika wote watakuwa wamesbabisha mradi huo kutofanikiwa waanze kuondoka kwa hiari yao.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alitoa siku mbili kwa uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kuhakikisha wanapeleka taarifa ya miradi
yote inayotekelezwa na gharama zake na muda wa kukamilisha mradi.
Alisema
kuwa hatua hiyo inataka kufanya Ofisi yake kuwa na uhakika wa thamani
halisi ya fedha na ubora wa mradi ili kuona kama kweli utawanufaisha
wananchi.
Naye
Mratibu wa Mradi wa Miombo Wilayani Kaliua Bennett Kamara alisema kuwa
taratibu zote za kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa na miombo
zinatolewa na Mkurugenzi Mtendaji ili ziunge mkono juhudi za wananchi
zilishakamilika muda mrefu lakini kwa muda mrefu fedha hizo bado ziko
ofisi ya Uhasibu.
Kwa
upande wa Katibu Tawala Msaidizi Dkt. Philip Ntiba alitoa wito kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kutoa haraka fedha mapema ili
kuwakatisha tamaa wananchi waliojitolea nguvu zao kuanzisha mradi huo.
0 comments:
Post a Comment