NA TIGANYA VINCENT-RS –TABORA
JUMLA
ya wakulima 4,268 wilayani Urambo wamejiandikisha kulima zao la Pamba
katika msimu wa kilimo unatarajia kuanza wakati wowote mwezi huu.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa wakati
akitoa taarifa ya maandalizi ya kilimo hocho kwenye ziara ya Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Aggrey ambaye anazungukia vijiji mbalimbali vinavyolima
pamba kwa ajili ya utoaji wa elimu juu ya ulimaji bora.Alisema
kuwa idadi ya wakulima wanatoka Kata 15 ambao wamo katika vijiji 49
wameleta makisio yao ya kulima zao hilo na kuongeza wakifanikiwa kulima
zinaweza kupatika zaidi tani 2000.
Kwingwa
alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri ambapo wanatarajia kupata
mbegu ambazo zimependekezwa na Bodi ya Pamba zisizokuwa na Manyoa tani
31.2 kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima kwa ajili ya kuanza kilimo
hicho.Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mwanri aliwaonya wakulima na wafanyabiashara
kutoingiza mbegu za manyoya ambazo zimepigwa marufuku na kuongeza kuwa
mkulima atakayepanda mbegu hizo atalazika kuzing’oa.
“Hapa
mbegu tutakayopanda ni UKM08 na sio nyingine …nikikutana mtu amepanda
mbegu iliyopigwa marufuku ya manyoa nitavuruga shamba lake na
kuwachukulia hatua watu ambao watakuwa wamebainika kuingiza mbegu hiyo”
alisisitiza Mwanri.
Alisema
kuwa wakulima wanatakiwa kuzingatia ushari wa kitaalamu ikiwemo umbali
kutoka shimo moja hadi jingine na mstari moja hadi mwingine ili waweze
kuwa na idadi ya miche inayotakiwa na 20,000 hadi 22,000 katika ekari
moja.
Mwanri
alisema kuwa idadi hiyo itawawezesha wakulima kupata kilo kuanzia 1000
hadi 1200 kwa ekari moja ambapo itakuwa ni zaidi ya zile walizokuwa
wakipata za 250 hadi 300 wakati wakilima bila kutumia utaalamu na mbegu
bora.Aliongeza
kuwa mtu yoyote atakayetaka kulima zao hilo ni vema akazingatia Sheria
na taratibu zinazoongoza zao hilo ili asije akajikuta katika matatizo ya
kushitakiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora yuko katika ziara maalumu ya kutembelea maeneo yote
yanayolima zao la pamba kutoka wilaya za igunga, Nzega, Uyui, Kaliua na
Urambo kwa lengo la kuwahamasisha watu washiriki kilimo hicho na vile
vile kutoa elimu juu ya kilimo bora kitakacho wasaidia kuzalisha mazao
mengi na ya ziada.
0 comments:
Post a Comment