Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa
Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange, akimkabidhi Mkuu wa
Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Angelina Kwinga mbegu ya mihogo
inayostahimili ukame katika uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hiyo ya
mihogo, mahindi aina ya Wema 2109 pamoja na viazi lishe yalioanzishwa
kwa ajili ya wakulima wa vijiji nane katika wilaya hiyo leo kwa ufadhili
wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana OFAB.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ugalla,
Geofrey Magambo akizungumza katika uzinduzi huo wakati akiwatambulisha
viongozi mbalimbali wa Kata hiyo na Kijiji cha Isongwa.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza katika uzinduzi huo.
Mshauri wa Jukwaa
la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange
(kulia), akizungumza kwenye uzinduzi darasa wa shamba la mahindi katika
Kijiji cha Isongwa kilichopo Kata ya Ugalla Ussoke wilayani Urambo
mkoani Tabora.
Mwakilishi wa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo.
Mwakilishi wa Mkuu
wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akikabidhiwa mbegu ya
mahindi ya Wema na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa
Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa.
Wananchi wa Kijiji cha Isongwa wakisubiri kupata mafunzo ya upandaji wa mbegu ya mahindi katika shamba darasa.
Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo
cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro akitoa maelezo kwa
wakulima wa Kijiji cha Isongwa jinsi ya kupanda mahindi aina ya Wema.
Mkulima wa Kijiji cha Isongwa, Malando Malando akiuliza swali.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni akiuliza swali.
Wanawake wakulima wa Kijiji cha Isongwa wakijumuika kwenye uzinduzi huo wakiwa na watoto wao.
Mtafiti, Ismail
Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro,
akionesha uchimbaji wa mashimo kabla ya kupanda mbegu hiyo ya mahindi.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni , akichimba mashimo.
Mtafiti, Ismail
Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro,
akionesha, akionesha namna ya kuweka mbolea kwenye mashimo
yaliyochimbwa.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo
ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akipanda
mahindi.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akipanda mahindi.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi, akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi huo.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo
cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza
wakulima wa Kijiji cha Usisya namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.
Wakulima wa Kijiji cha Kapiluka wakijiandaa kupanda mbegu ya viazi lishe.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo
cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza
wakulima wa Kijiji cha Motomoto namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.
Na Dotto Mwaibale, Urambo Tabora
TAFITI za kilimo zinazofanywa hapa
nchini na wataalamu zimewafikia wakulima wa Wilaya ya Urambo mkoani
Tabora kwa mara ya kwanza.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa
Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi wakati akizungumza na waandishi
wa habari kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema
2109 na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji nane
vya Isongwa, Ussoke, Usisya, Kapiluka, Vumilia, Kamalendi, Muungano na
Songambele.
Alisema mara nyingi tafiti zilizokuwa
zikifanyika zilikuwa zikibaki kwenye makabati bila ya kuwafikia walengwa
na jambo lililofanywa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya
Kilimo (OFAB) kuwafikishia wakulima matokeo ya tafiti hizo ni jambo zuri
na limefurahiwa na kwa hapa kwetu ni mara ya kwanza kutokea.
"Tuna amini kuwa hivi sasa uchumi
utastawi kuanzia ngazi ya familia, wilaya na hadi taifa na tutakuwa na
chakula cha kutosha" alisema Malunkwi.
Malunkwi alisema katika wilaya hiyo
walikuwa na changamoto kubwa ya kupata mbegu bora kwani wakulima wengi
walikuwa wakitumia mbegu za zamani walizozizoea na kujikuta wakipata
mazao kiduchu lakini kwa ujio wa mbegu hizo ni ukombozi mkubwa kwao.
Alitaja changamoto nyingine ambayo
inapaswa kuangaliwa kwa karibu kuwa ni bei kubwa ya mbegu hiyo ya
mahindi ambayo inauzwa shilingi 12,000 kwa kilo mbili huku kukiwa na
debe moja la mahindi linalouzwa shilingi 10,000 ambalo wakulima wamekuwa
wakilikimbilia kutokana na bei yake kuwa ya chini ingawa mazao yake
hayana tija.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema
mbegu hiyo ya mahindi imefanyiwa utafiti na inavumilia ukame wakati ile
ya mihogo ikivumilia magonjwa kama batobato na michirizi kahawia huku
zikitoa mavuno mengi.
Alisema COSTECH katika mkoa huo imetoa
kilo 60 za mbegu ya Wema, mihogo 40,000 na viazi lishe 75 ambapo katika
wilaya hiyo vijiji nane vimenufaika kwa ajili ya kutengeneza mashamba
darasa ambayo yatatoa mbegu zitakazosambazwa kwa wakulima katika maeneo
mengine.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora
katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi
Uchumi, Phillips Mtiba alisema hivi sasa mwajiriwa ni mkulima ambaye
analima kilimo chenye tija na si vinginevyo na kuwa serikali siku zote
imekuwa ikihimiza kilimo bora ambapo aliwataka maofisa ugani kupanga
ratiba za kuwafikia wakulima.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Angelina Kwinga
aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kutekeleza ahadi ya kuwapelekea mbegu
kama walivyo ahidi walipokuwa wakitoa mafunzo kwa maofisa ugani wa
wilaya hiyo mapema mwaka huu.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
0 comments:
Post a Comment