NA TIGANYA VINCENT
2 NOVEMBA 2017
RS-Tabora
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imetoa onyo kwa Kampuni zote za usambazaji pembejeo
za zao la Pamba kuhakikisha mbegu na dawa za kuua wadudu watakazopeleka
kwa wakulima ni bora na hazina matatizo ili zisije zikawasababishia
hasara wakulima.
Onyo
hilo limetolewa jana wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri wakati wa mkutano wa kuwaelimisha wakulima juu ya kulima zao hilo
kwa kufuata Sheria na Taratibu zake ili kuongeza ubora.
Alisema
kuwa Kampuni hizo zilizopewa kazi ya kusambaza Mbegu kwa wakulima wa
pamba katika Wilaya Tano za Mkoa huo ni vema zikapeleka mbegu bora na
zilizopendekezwa kulima zao hilo ni vema zikahakikisha kuwa zinapeleka
kwa wakulima mbegu iliyopendekezwa ya UKM08 ambayo iko katika ubora na
wakawa na uhakika kuwa inatoa ili kuwaepusha wakulima kupoteza nguvu
zao.
Mwanri
aliongeza kuwa na ni vema wakahakikisha dawa watakazosambaza kwa
wakulima wa Pamba katika maeneo ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuua
wadudu zikawa ni zile zilizopendekezwa na zina uwezo kweli wa kuua
wadudu haribifu na kuongeza kuwa kinyume cha hapa atawakamata wao na
wali zao ili waweze kufidia hasara kwa mkulima.
“Najua
nyie Kampuni zilizopewa jukumu la kusamabaza mbegu kwa wakulima na dawa
mtapeleka mbegu bora na zilizokubalika…ikitokea kuwa mbegu mlisambaza
kwa wakulima zikashindwa kuota na dawa ikashindwa kuua wadudu…mimi
nitakachofanya ni kukamata mali zenu zote ili ziuzwe kufidia hasara
ambayo wakulima watakuwa wamepata “ alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Alisema
kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa anabeba dhamana ya kuhakikisha kuwa hakuna
mkulima yoyote anapata hasara kwa sababu za makusudi au uzembe wa
watendaji wowote wale bali yuko pale kuwashika mkono wakulima.
Kwa
upande wa Meneja kutoka Kampuni ya Quton Tanzania limited iliyozalisha
Mbegu zinazosambazwa katika maeneo mbalimbali Phineas Chikaura alisema
kuwa mbegu hiyo inasambazwa katika maeneo mbalimbali katika Wilaya
yaNzega inao ubora ambao umedhibitishwa na Taasisi ya utafiti wa Mbegu
hapa nchini.
Alisema
kuwa kinachotakiwa kwa mkulima wa pamba ni pamoja na kufuata kanuni za
upandaji wake ikiwa ni pamoja na shimo kutozidi urefu wa sentimeta tatu
na mbegu kutolowekwa kama baadhi wanavyofanya.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameziagiza Kampuni hizo zinazosambaza
Mbegu kahakikisha Mbegu na vifaa vyote vinavyotakiwa kwa mkulima kuanza
kupanda vinafika kwa mkulima ndani ya siku 10 zijazo.
Alisema
kuwa nje ya hapo mvua zikianza kunyesha upo uwezekana wa mbegu
kuchelewa kumfikia mkulima na hivyo kushindwa kulima na kumkatisha
tamaa.
Mwanri
aliwaagiza Maafisa Ugani wote kuhakikisha wanajipanga vizuri ili
kufuatilia kama kweli wakulima wote wamepata mbegu kwa wakati.
Wakati
huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku mizani ya rula kutumika
wakati wa zoezi la ununuzi wa pamba katika enro hilo badala yake alisema
kuwa utakaokuwa unatumika ni ule wa dijitali.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuondoa wizi ambao wakulima wamekuwa
wakifanyiwa kupitia mizani ya rura na kuwafanya kupata mapato kidogo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora yuko katika ziara ya kutembelea wilaya zote
zinazolima Pamba ambazo ni Igunga, Nzega, Uyui, Urambao na Kaliua
kuwahamasisha wakulima kulima kilimo cha kisasa na kuondokana na tabia
ya kuchafua pamba ili waweze kupata bei nzuri
0 comments:
Post a Comment