Home » » DC AVALIA NJUGA WATOTO KUTUMIKISHWA

DC AVALIA NJUGA WATOTO KUTUMIKISHWA

na Hastin Liumba, Sikonge
SERIKALI mkoani Tabora imeyataka makampuni yanayojishughulisha kilimo cha tumbaku na yale yanayopinga utumikishwaji watoto mashambani, kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule na kupata fursa ya kupata elimu.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, kwenye maadhimisho ya sherehe za kupinga utumikishwaji wa watoto katika mashamba ya tumbaku zilizofanyika katika Kata ya Mole, wilayani Sikonge.
Alisema, serikali ya mkoa wa Tabora itasimamia kwa karibu, na ipo tayari kuhakikisha sheria za kupinga utumikishwaji wa watoto zinafuatwa.
“Watoto hawakuumbwa waje kuteseka duniani kwani kutumikisha watoto ni dhambi tena dhambi kubwa.” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa sera wa mradi wa PROSPER, Mary Kibogoya, akitoa taarifa ya historia ya siku ya kutokomeza utumikishwaji wa watoto, alisema sherehe hizo hufanyika Juni 12 ya kila mwaka ulimwenguni kote.
Kibogoya alifafanua kuwa, mradi wa kutokomeza utumikishwaji wa watoto katika mashamba ya tumbaku (PROSPER), unafadhiliwa na shirikisho la makampuni ya tumbaku ulimwenguni (ECLT) kupitia Winrock international.
Aidha, alisema kampuni nyingine ambazo zinazoshirikiana nao kukomesha utumikishwaji watoto kwenye mashamba ya tumbaku, ni shirika la maendeleo la mkoani Tabora (TDFT).
Naye Mkurugenzi wa mradi wa PROSPER, Bahati Nzunda, alisema mradi huo umelenga kufanya shughuli mbalimbali kama vile kusaidia watoto kielimu hadi kufikia watoto 1,800 waliopo shule za msingi.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa