Home » » Rage atoa msaada wa vifaa vya michezo vya sh. Milioni 12

Rage atoa msaada wa vifaa vya michezo vya sh. Milioni 12

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba,Ismail Rage,ametoa vifaa vya michezo kwa timu za Manispaa ya Tabora vyenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 12.

Akikabidhi vifaa hivyo,Rage ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Amesema vitatumika kuendeleza mchezo wa mpira wa Miguu katika manispaa ya Tabora.

Amesema michezo mbali ya kuwa ni furaha na afya lakini inatumika kuwaweka pamoja vijana wenye itikadi mbalimbali za siasa na kuwafanya wawe ndugu hivyo kuondoa uhasama miongoni mwao.

Kwa upande wao wawakilishi waliopewa vifaa vya michezo,wamempongeza Mwenyekiti huyo wa simba na kwamba watavitumia kuendeleza na kuibua vipaji vya vijana kwenye maeneo yao.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mipira,seti za jezi,soksi ishirini na saba ambazo zimetolewa kwa vijana katika Manispaa ya tabora.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa