MKOA wa Tabora una idadi
kubwa ya wagonjwa wa Kiharusi ingawa wengi hawajitokezi kupata tiba Hospitalini
badala yake wanatibiwa nyumbani.
Mganga mkuu wa Mkoa wa
Tabora,Dk.Leslie mhina,amesema kumekuwa na wagonjwa wengi wa kiharusi Mkoani
Tabora hali ambayo mwanzoni walidhani tatizo sio kubwa.
Amesema Kiharusi ni
tatizo kubwa na hilo wamebaini baada ya kugundua idadi kubwa ya wagonjwa wa
kiharusi wanatibiwa kienyeji wakiwa majumbani huku tiba kubwa ikiwa ni
kufukuziwa mavi ya tembo.
Amesema wananchi wengi
hawaamini kama Kiharusi kinatibiwa hospitalini endapo matibabu yatafanyika
mapema na kuwataka wananchi kuwawahisha wagonjwa ili wapate tiba haraka na sio
kukimbilia kuwatibu kienyeji.
0 comments:
Post a Comment