Home » » Dk. Kafumu awaonya watendaji wa serikali

Dk. Kafumu awaonya watendaji wa serikali

MBUNGE wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Dk.Peter Dalaly Kafumu amesema hatamvumilia kiongozi yeyote wa serikali ambaye ataonekana kuwa kikwazo katika shughuli za maendeleo. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa hoteli ya The pick wilayani hapa.
Dk.Kafumu alisema baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa hawatekelezi majukumu yao ipasavyo na kusababisha serikali kuonekana kuwa haifanyi kazi.

Alisema baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wakifanya kazi kwa maslahi yao binafsi na kujihusisha na masuala ya siasa.

Suala hilo linaleta mgawanyiko kwa wananchi na kurudisha nyumba kasi ya maendeleo, alisema.

Alisema katika miezi mitatu alipoingia madarakani kabla hajatenguliwa ubunge aliweza kutoa kipaumbele katika suala la afya.

Dk. Kafumu alisema alitoa msaada wa vitanda 300 katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga kwa lengo la kusaidia akinamama wajawazito pamoja na pikipiki mbili kwa jeshi la polisi.

Alisema katika kipindi hicho kifupi cha uongozi wake aliweza kusimamia na kutoa ushauri katika masuala ya ardhi ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa Wilaya ya Igunga.




CHANZO GAZETI LA MTANZANIA 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa