na
Thomas Murugwa, Tabora
MAOFISA wa Uhamiaji mkoani Tabora wanamshikilia
raia wa Burundi kwa tuhuma za kuwasafirisha watoto saba kwa lengo la kuwafanyia
biashara.
Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tabora, Danson
Mwakipesile, alimtaja mtu huyo kuwa ni Emmanuel John (22) ambaye pia ni raia wa
Rwanda.
Alisema mtu huyo alikamatwa eneo la Ulyankulu,
Wilaya ya Kaliua, akiwa na watoto hao saba wenye umri kati ya miaka 12 na 14
ambao nao pia ni raia wa nchi nchi hizo.
“Tulimkamata akiwa hana vibali akiwa na watoto saba
kutoka nchi jirani wakiwa na umri usiozidi miaka 14,” alisema.
Mwakipesile alisema watoto hao watatumika kama
mashahidi pindi mtu huyo atakapofikishwa mahakamani.
Aliwataja watoto hao waliokuwa wakisafirishwa kuwa
ni Ndayisenga Batiliza, Ndakusenga Emmanuel, Nimbonajile Nagenda, Yazid John,
James Justus na Samson Banteze.
Mwakipesile alisema mtu huyo atafunguliwa mashtaka
ya kuingia nchini isivyo halali na kufanya biashara ya binadamu.
Alisema hivi sasa wameweza kudhibiti wimbi kubwa la
wahamiaji, lakini wanaoleta usumbufu ni wakulima wa zao la tumbaku ambao
hupenda kuwatumia watoto wadogo kwenye kilimo huku wakiwalipa ujira kidogo.
Wakizungumzia kuletwa kwao nchini, watoto hao
walidai waliambiwa na mtu huyo kuwa anawaleta kwa lengo la kufanya kazi kwa
mshahara wa sh kati ya 30,000 hadi sh 50,000
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment