WANACHUO katika
chuo cha Kilimo na mifugo Tumbi,Mkoani Tabora wamepongezwa kwa kufanya vizuri
katika mitihani ya kumaliza masomo yao chuoni hapo ambapo zaidi ya asilimia 95
wamefaulu.
Akitoa
pongezi kwa wanachuo waliomaliza mwaka huu,mwenyekiti wa bodi ya chuo
hicho,Bw.Omary Kamulika, amesema kati ya wanachuo 412 waliomaliza mafunzo
katika ngazi ya Cheti, wanachuo 401 wamefaulu masomo yao huku kumi na moja wakitakiwa
kurudia.
Amesema
wanachuo waliomaliza ni lazima wapongezwe kwani pamoja na kukabiliwa na
changamoto nyingi lakini wameweza kufanya vema.
Bw,Kamulika
amewahakikishia wananchi na wanachuo kwa ujumla kuwa Chuo cha kilimo na mifugo
Tumbi kitaendelea kuwa Chuo bora katika kuwaandaa wanachuo ili wawe watumishi
wazuri watakaolifaa Taifa.
Kuanzia
mwaka huu wa masomo 2013/14 Chuo hicho kitaanza kuchukua wanafunzi wa Diploma
wapatao Mia Moja na hamsini huku wale wa ngazi ya cheti wakiwa Mia nne.
0 comments:
Post a Comment