Home » » Ajinyonga baada ya kufeli mtihani wa mwisho wa ualimu

Ajinyonga baada ya kufeli mtihani wa mwisho wa ualimu


Na Diana Rubanguka, Kigoma.
MWANAFUNZI wa chuo cha Ualimu Tabora amekutwa amejinyonga katika eneo la Burega lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Freisser Kashai amesema kuwa mnamo Julai 31 mwaka huu majira ya saa 3:30 asubuh katika eneo hilo mwanafunzi huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya nailon akiwa chumbani kwake.
Kamanda Kashai alimtaja Marehemu kuwa ni Moses Iddi (28) Mnyamwezi ambapo baada ya tukio hilo alifariki dunia bila kupata msaada wowote
Amesema kuwa chanzo cha kujinyonga kwake ni kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wake wa kumaliza kozi ya ualimu daraja A katika chuo hicho kilichopo Mkoani Tabora.
Kamanda kashai alisema kuwa awali kabla ya kujinyonga aliacha ujumbe wa maandishi uliosema kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa