WATENDAJI wa Vijiji
na Kata wilayani uyui, wameonywa kuwa kama hawataitisha vikao vya kueleza
taarifa za mapato na matumizi,hawataruhusiwa kutumia pesa.
Akifungua mafunzo
elekezi kwa watendaji wa Kata,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Tabora,Uyuni Said Ntahondi amesema kuanzia sasa hilo litazingatiwa na pia hatua
za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Amebainisha kwamba
vikao vya kutoa taarifa za mapato na matumizi ni muhimu kwa vile vinarudisha
imani ya wananchi katika kuchangia miradi ya maendeleo.
Kwa upande wao watendaji
hao wameeleza ili waweze kutimiza majukumu yao kikamilifu ni lazima wawezeshwe
kwa vitendea kazi kwa vile wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazowakwamisha
katika utendaji wao wa kazi.
Naye afisa utumishi
wa Halmashauri hiyo Ahmada Suleiman amesema lengo la mafunzo hayo ni
kuwawezesha watendaji hao wa Kata watekeleze majukumu yao kikamilifu na sio
kufanya kazi kwa mazoea.
0 comments:
Post a Comment