WANANCHI Wilayani
Urambo wamehimizwa kupanda miti kwa wingi ili kutunza mazingira kwa vile zao la
tumbaku linatumia kuni nyingi.
Akizindua hifadhi ya
Misitu ya Halmashauri ya wilaya ya Urambo, Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru,
Juma All Simai,amesema kutokana na zao la tumbaku kutumia sana kuni kukaushia
tumbaku ni lazima wananchi wawe mstari wa mbele kupanda miti kwa wingi na
kutunza mazingira.
Amesema kama
wasipotunza mazingira kwa kupanda miti,watakabiliwa na jangwa lakini pia kukosa
nishati ya kukaushia tumbaku yao.
Akiweka jiwe la mingi
Shule ya Msingi ya Santa Maria,Kiongozi huyo amepongeza uwekezaji katika elimu
na hasa mipango ya uongozi wa shule hiyo baadae kuwa na Chuo cha ualimu,akisema
itasaidia kupunguza zaidi tatizo la walimu wilayani Urambo.
Awali Mkurugenzi wa
Shule hiyo,Emmanuel Soko,alisema mipango ya shule yake ni kutoa elimu bora
kuanzia shule ya msingi,sekondari na baadae Chuo cha Ualimu ili vijana
watakaokuwa wanamaliza shuleni hapo wanaopenda kuwa walimu wajiunge na
kufundisha katika mazingira waliyokulia na kuyazoea.
0 comments:
Post a Comment