Katibu
tawala mkoa wa Tabora, Kudra Mwinyijuma akizungumza kwenye hafla ya
kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Protace
Magayane Kwa sasa Magayane ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Ikungi mkoa wa Singida. Pia katika hafla hiyo iliyofanyika Igunga
mjini,mkurugenzi mpya wa halmashauri ya Igunga, mwalimu Rustika Turuka
alikaribishwa rasmi.Wa kwanza kulia (walioketi) ni mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Protace Mgayane na anayefuatia ni
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Abubakari Shaban.
Katibu
tawala mkoa wa Tabora, Kudra Mwinyijuma (kulia) akimkabidhi mweka
hazina wa halmashauri ya wilaya ya Igunga,Gordon Julius Dinga,cheti
maalum baada kuiwezesha halmashauri hiyo kupata hati safa ya mahesabu
kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2010/2011 na 2011/2012.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Abubakari Shaban
akitoa nasaha zake kwenye halfla iliyofana ya kumuaga aliyekuwa
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Protace Magayane
aliyehamia wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida. Pia kumkaribisha mkurugenzi
mpya wa halmashauri ya Igunga, mwalimu Rustika Taruka.Wa pili kushoto
ni mkurugenzi Protace Magayane na wa kwanza kushoto ni mke wake
mkurugenzi Magayane.
Aliyekuwa
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga,Protace Magayane akitoa
nasaha zake wakati akizungumza kwenye hafla ya yeye kuagwa na viongozi
na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga.
Mkurugenzi
wa halmashauri mpya ya Ikungi mkoa wa Singida, Protace Magayane
(kushoto) akijadiliana mambo ya Afisa wake wa Kilimo Ayubu Sengo wakati
wa hafla ya kuagwa (Magayane) iliyofanyika Igunga mjini.
Baadhi
ya viongozi na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoa wa
Tabora, wakipata msosi kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Igunga, Protace Magayane na kumkaribisha
mkurugenzi mpya wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, mwalimu Rustika
Turuka.Hafla hiyo ilifanyika Igunga mjini.
Mtaalam
wa kufungua champeni wa wilaya ya Igunga ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja akifungua Shampeni kwenye hafla ya kumuaga
aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Protace
Magayane na kumkaribisha mkurugenzi mpya mwalimu Rustika Turuka.
SERIKALI mkoa wa Tabora,imewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya na Manispaa,kusimamia kikamilifu matumizi ya mali za umma ikiwemo fedha, kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za nchi.
Hatua hiyo itasaidia pamoja na mambo mengine,Halmashauri kupata hati safi za mahesabu ya fedha za umma.
Changamoto hiyo imetolewa juzi na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora,Kudra Mwinyimvua,wakati akizungumza kwenye sherehe ya kupongezana watumishi wa Halmashauri ya Igunga kwa kupata hati safi kwa miaka miwili mfululizo (2010/2011 na 2011/2012).
Alisema dawa pekee ya kuwa na uhakika wa halmashauri kupata hati safi,ni kuimarisha usimamizi wa ndani wa matumizi ya mali za umma ikiwemo fedha za umma.
Mwinyimvua alisema usimamizi huo pia utasaidia utoaji huduma bora zitakazokidhi matarajio ya wananchi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi kuwa ubora unaofanana na fedha za umma zilizotumika.
“Kwa halmashauri ya Igunga,nitumie jioni hii kuwapongeza kwa dhati kabisa madiwani na watendaji kwa juhudi zao zilizofanikisha halmashauri kupata hati safi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo”,alisema katibu tawala huyo na kuongeza;
“Pongezi pekee zimwendee Mkurugenzi Protace Magayane (kwa sasa amehamishiwa halmashauri ya Ikungi mkoa wa Singida) kwa juhudi zake binafsi za kuwaunganisha madiwani na watendaji kufanya kazi za umma kama mnyororo kitendo kilichosaidia kuiletea halmashauri maendeleo endelevu”.
Aidha,Mwinyimvua alitumia fursa hiyo kumtakia kila la kheri mkurugenzi Magayane katika kuwatumikia wananchi wa wilaya mpya ya Ikungi mkoani Singida.
Sherehe hiyo iliyofana ilitumika pia kumuaga mkurugenzi Magayane aliyehamia wilaya ya Ikungi na kumkaribisha mkurugenzi mpya mwalimu Rustika Turuka

CHANZO BLOG YA SINGIDA
0 comments:
Post a Comment