Home » » Kinana awashukia wafanyabiashara

Kinana awashukia wafanyabiashara

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewashukia wafanyabisha wanaotumia fedha zao kwa lengo la kutaka kujinufaisha na kuona kuwa ni pango la kuficha maovu yao. Amesema kutokana na hali hiyo ni lazima viongozi wa ngazi za wilaya na mkoa wahakikishe wanaweka wazi mikataba yote ya majengo ya biashara hali itakayosaidia kujengeka kwa imani kwa wanachama wake.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa alipozindua mradi wa vibanda vya biashara 54 vilivyojengwa kwenye uwanja wa Samora.

Alisema ni lazima CCM ijitegemee kwa kutegemea rasilimali zake badala ya kutegemea watu kila wakati.

Kinana alisema hivi sasa kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakijitokeza kufadhili masuala mbalimbali lakini ndani yake wamekuwa na malengo ya kujinufaisha huku wakitumia kivuli cha CCM.

“Sasa kutokana na hali hii ni lazima kila kiongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya ahakikishe mitakaba yote iko wazi. Leo hii kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kufadhili masuala mbalimbali ya kumbe ndani yake wamekiwa wakijinufaisha kwa kivuli cha CCM,” alisema.

Awali Katibu wa Uchumi wilaya ya Nzega, Majaliwa Bilal, alisema ujenzi huo wa vibanda 54 umewashirikisha wananchi ambao wamepewa maeneo hayo kwa maslahi ya chama.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa