Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011 yatakiwa kuanza kutumika
SHERIA
ya manunuzi ya mwaka 2004 imeelezwa kuwa inatakiwa iachwe kutumiwa na
badala yake ile ya mwaka 2011 ianze kutumika haraka kwani ina manufaa
makubwa.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Tabora,Uyui,Mh Said Ntahondi amesema sheria
ya mwaka 2004 ina mapungufu yanayopelekea pesa nyingi kutumika katika
miradi ya maendeleo huku mchakato wake ukiwa ni mrefu pesa ambazo
zingeweza kukokolewa na kutumika katika shughuli zingine za maendeleo
Akizungumzia
mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Makao makuu ya wilaya ya
Uyui,Isikizya,Mwenyekiti huyo amesema sheria ya manunuzi ya mwaka 2011
ina manufaa makubwa ukilinganisha na ile ya mwaka 2004.
Mheshimiwa
Ntahondi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ilolangulu,amesema kwa kutumia
njia ya manunuzi ya moja kwa moja badala ya mkandarasi wameokoa zaidi
ya asilimia Arobaini ya gharama za ujenzi wa kituo cha Polisi kwani
kilikuwa kitumie shilingi zaidi ya Milioni Mia tatu lakini kwa kutumia
manunuzi ya moja kwa moja wameokoa zaidi ya shilingi Milioni Mia Moja na
Hamsini.
Halmashauri ya wilaya ya Tabora,Uyui imejipanga kupiga hatua
kimaendeleo na kuboresha Makao yake makuu kwa majengo yenye ubora
unaokubalika.
0 comments:
Post a Comment