Home » » MSAADA WAKO UNAHITAJIKA: "Namtafuta mama yangu niendelee masomo.‏" -Zaituni Rashid Kaige

MSAADA WAKO UNAHITAJIKA: "Namtafuta mama yangu niendelee masomo.‏" -Zaituni Rashid Kaige

Zaituni Rashid Kaige kushoto akiwa rafiki zake wilayani
Sikonge mkoani Tabora anakoishi sasa.

…NINA matumaini na kutamani sana kuwa siku moja nikimpata mama yangu
mzazi nadhani nitakuwa kama nimezaliwa upya na nitaendelea na masomo
na kutimiza ndoto zangu za maisha”.
 
Hayo ni maneno ya Zaituni Seif Kaige,(20) mkazi wa wilaya ya Sikonge
mkoani Tabora alitoa maneno hayo wakati akizungumza na mwandishi wa
makala hii wilayani humo.
 
Kaige alisema amefikia hatua ya kumtafuta mama yake kwa njia hii ili
aweze kufikia malengo yake kimaisha hususani kujipatia elimu kwani
hatua aliyofikia anaona bado kuna kiza kinene mbele yake.
 
Anasema alipotezana na mama yake toka mwaka 2000 wakiwa Kiloleni
mkoani Tabora akiwa na umri wa miaka saba baada ya kutokea tofauti
kati ya mama na baba yake aitwaye Seif Rashid Kaige ambaye ni mtumishi
wa shirika la Tanesco wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
 
Aidha anasema hadi sasa licha kumtafuta mama yake mzazi aitwaye Sabina
Malekela amefanikiwa kupata elimu ya kidato cha nne katika shule ya
sekondari Ngulu iliyoko wilaya ya Sikonge lakini ameona endapo
akimpata mama yake mzazi anataka kuendelea na masomo.
 
“Mama aliondoka tukiwa mkoani Tabora eneo la kata ya Kiloleni manispaa
Tabora…..toka ameondoka sijapata kumuona tena wala kusikia hata alipo
ninajisikia uchungu sana kutomjua mama yangu japokuwa siku nikimuona
ninaweza kumtambua kwa sura…naumia mno kila ninapomuwaza na
kumkumbuka.”anasema.
 
Anasema kibaya zaidi sijapata kumfahamu ndugu wa mama yangu hata mmoja
labda ningefanikiwa kujua alipo lakini baba yangu alinieleza kuwa nina
mjomba wangu aitwaye Hamis Malekela aishiye mkoani Dodoma.
 
“Baba aliwahi kunieleza kuwa nina mjomba wangu aishiye mkoani Dodoma
eneo la Mtera Kota lakini sina uwezo wa kufika huko hali ambayo
inaniwia vigumu hadi kuamua kutumia njia hii ya gazeti kwani nina
imani sauti yangu itafika mbali.” anaongeza.
 
Alisema namba za mama wala za ndugu wa mama yake hana hivyo ni kitu
kinachomuwia vigumu wapi aanzie kumtafu wake.
 
Aliongeza na kushauri kuwa anapenda familia zote zifikie mahali ziwe
na muono kuhusu malezi sahihi na stahiki ili kuweza kutengeneza
familia zenye maadili mema ya kiroho na kimaadili.
 
Anaeleza kuwa wanawake na hata wanaume wanayo haki sawa ya kuishi na
kupewa heshima kama ilivyo kwa binadamu yoyote na anasema haya kwa
sababu anajua anachomaanisha katika maisha yake.
 
Anafafanua kuwa licha ya kuwa katika umri mdogo na elimu duni
aliyonayo lakini anatambua kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania katika kifungu cha 14 na 16 kinaeleza wazi kuwa
kila mtu anayo haki ya kuishi na kuheshimiwa utu wake.
 
Anasema bado nchi yetu inakabiliwa na changamoto za malezi kiasi cha
familia nyingi kushindwa kulea familia ama watoto hasa katika suala
zima la elimu kwa watoto wa kike.
 
Endapo atampata mama yake.
 
Kaige anasema endapo atafanikiwa kumpata mama yake mzazi angependa
kuendelea na masomo ili kufikia malengo yake kimaisha kwani elimu
aliyonayo ya kidato cha nne bado anaona hajafanya chochote mbele ya
maisha ya sasa yenye kila aina ya uhitaji wa sayansi na teknolojia
duniani.
 
Anaongeza licha ya kutambua umuhimu wa elimu bado anaona itakuwa ni
njia sahihi ya kusaidia familia yake hususani mama yake mzazi kwani
anampenda sana kwani anatamani sana kuwa mwanasayansi kutokana na somo
hilo kulipenda zaidi.
 
Anasema ametafuta fursa ya kujiendeleza kielimu kwa muda sasa lakini
aliikosa na endapo atampata mama yake ndoto za maisha mpya zitafufuka
kwani vyama vya hiari vya kijamii nchini vimekuwa vikipigania sheria
kandamizi zinazowanyima wanawake fursa za kujieletea maendeleo
hususani elimu.
 
“Naamini kuwa matatizo yanawakumba watoto wa kike ama wanawake ni
matokeo ya jamii kukumbatia sheria na utamaduni uliopitwa na
wakati…..kinachonitokea ni halisia ya jambo hili leo hii sina elimu
ninayoitafuta kwa kukosa msaada ninaoutaka katika kutafuta elimu.”
anafafanua Zaituni Kaige.
 
Anasema kila akikaa anafikiria ni jinsi gani ataweza kuwa mtumishi
siku moja hasa kutokana na elimu ya kidato cha nne,elimu ambayo haina
chochote kile cha kuweza kuajiriwa ama kujiajiri.
 
Kaige anafafanua kuwa bado anaona kuwa suala la usawa wa jinsia kwa
nchi yetu ndani ya familia linahitaji msukumo na kungaliwa kwa umakini
kwani watoto wengi wa kike wanashindwa kusoma kutokana na mitihani
mingi wanayopata kwenye mzunguko wa maisha.
 
“Haya ndiyo matokeo ya mfumo dume kwa maisha ya nchi hasa za
Afrika....haitasaidia nchi yetu kupiga hatua kwenye maendeleo.”
aliongeza.
 
Bado anapenda kusoma.
 
Anasema licha kuishia kidato cha nne lakini bado anapenda kusoma ili
kuweza kufikia anakotaka.
 
Anafafanua kuwa licha kutaka elimu zaidi bado masomo ambayo anayapenda
toka akiwa shule ni Historia, Jiografia, English na Hisabati, lakini
bado kati ya masomo hayo baadhi yalihitaji kufundishwa zaidi.
 
“Napenda kusoma nikimpata mama najua nitakuwa nimeutua mzigo wa kukosa
elimu….naamini elimu ndiyo kila kitu duniani kwa sasa hasa kwa mtoto
kama wa kike.”anasema.
 
Zaituni Kaige anasema endapo kama kuna msamaria mwema atapata ama ana
taarifa alipo mama yake mzazi amtafute kwa namba hizi za mtandao wa
Vodacom 0755-165972 au Airtel 0785-175258.
 
Anasema ana imani Mwenyezi Mungu siku moja atamkutanisha na mama yake
mzazi na hapo ndipo utakuwa mwanzo wa maisha yangu kueleka mafanikio
au ‘Nitazaliwa Upya.’
 
Pix namba 150 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa