Home » » Chama cha Msingi chatenga fedha kwa ajili ya kuweka umeme

Chama cha Msingi chatenga fedha kwa ajili ya kuweka umeme

CHAMA Cha Msingi cha Wakulima wa Tumbaku, kata ya Kisanga
wilayani Sikonge, kimetenga Shilingi Milioni 5  za mauzo ya
tumbaku kwa msimu wa 2013/2014 kwa ajili ya kutunisha mfuko maalumu wa kuweka umeme kwenye vijiji vitatu.

Mwenyekiti wa Chama hicho Rashid Mazinge,amesema chama hicho chenye jumla ya wanachama 700 kimekusudia kuweka umeme  Makao makuu ya kata hiyo yaliyoko  kijiji cha Kisanga na vijiji vingine.

Amesema wametenga fedha hizo kwa ajili ya maandalizi
ya awali ambapo wataanza kwa kununua vifaa mbalimbali vinavyotumia umeme  vitakavyosaidia kurahisisha shughuli mbalimbali za kiofisi katika ofisi ya chama hicho.

Katika msimu wa 2012/2013 chama hicho kilizalisha jumla ya kilo
940,049 za tumbaku zenye thamani ya Shilingi Bilioni  4.1 na mapato ya ushuru yalikuwa Shilingi Milioni 103.4 ambapo waliweza kulipa deni la pembejeo la shilingi Shilingi Bilioni 1.1 kutoka Benki ya NMB.

Msimu wa 2013/2014 walilenga kuzalisha jumla ya kilo Milioni
1.4 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.3 na mapato ya ushuru walilenga kukusanya Shilingi Milioni 156.8 hali ambayo itawawezesha kulipa deni la pembejeo la Shilingi Bilioni 1.5 toka NMB.

Diwani wa kata hiyo, Abdallah Msumeno mbali na kupongeza hatua ya chama hicho kutenga Shilingi Milioni 2 kwa ajili ya kununua viti 100 vya plastic na kutenga Shilingi 576,000 za michango ya wanachama wa NSSF pia ametoa wito kwa wakulima hao kufuata kalenda ya msimu wa kilimo ili kilimo chao kiwe na tija na kupata mafanikio zaidi.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa