MTAALA mpya wa Masomo wa Chuo
cha Ardhi Tabora utawezesha Chuo hicho kutoa wahitimu wenye uwezo wa kufanya
kazi bila matatizo tofauti na ilivyo sasa.
Akifunga mafunzo ya
Mtaala Mpya wa chuo hicho,Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora,Bw.Longino
Kazimoto,ameagiza Chuo hicho kisajiliwe haraka na NACTE ili mtaala mpya
utakapoanza kutumika usaidie kupatikana wahitimu wenye uwezo wa kufanya kazi.
Mkuu wa Taaluma wa
Chuo hicho,Bi.Helena Kenekeza,amesema lengo la mafunzo ni
kukamilisha Mtaala mpya ili wanachuo wanapomaliza wawe mahiri katika kazi zao
na wasitegemee mafunzo kazini kama ilivyo sasa.
Kwa upande wao wadau
wa mafunzo hayo wamesifu Mtaalama huo Mpya utakaoanza kutumika kuwa utakifanya
Chuo kuwa na sifa nzuri kwani kitakuwa na uwezo wa kutoa wahitimu wenye ubora
wanaojua kufanya kazi.
Chuo cha Ardhi Tabora
kinatoa mafunzo katika ngazi ya Cheti na Stashahada katika fani mbalimbali za
Ardhi,kikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa uzio,Nyumba za watumishi,Gari na
zahanati kwa ajili ya kuwahudumia wanachuo na watumishi.
0 comments:
Post a Comment