Na Hastin Liumba,Nzega
HALMASHAURI NZEGA KUTUMIA BILIONI 35.4 2014/2015.
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora
imeomba kuidhinishiwa kiasi cha sh 35,455,837,199 kwa mwaka wa fedha
wa 2014/2015.
Akisoma taarifa ya bajeti hiyo kaimu afisa mipango wa halmashauri hiyo
Martin Jakanyango alisema kiasi hichi kinajumuisha sh 1,378,203,500
kama vyanzo vya ndani vya halmashauri.
Jakanyango aliongea kiasi cha sh 579,594,000 ruzuku ya fidia ya
kodi,ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya mishahara 23,978,711,716.
Aidha aliongeza kuwa sh 2,911,348,000 ni ruzuku kwa ajili ya matumizi
ya kawaida,ruzuku kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni sh
5,326,293,982,ruzuku kwa ajili ya mifuko ya pamoja ni sh 1,231,686,001
na michango ya wahisani sh 50,000,000.
Wakati huo huo baraza hilo lilipitisha bajeti ya halmashauri ya mji
mdogo Nzega kiasi cha sh 1,012,372,763 kwa mwaka wa fedha wa
2014/2015.
Taarifa hiyo inasema kiasi cha sh 1,228,220,000 kitatokana na vyanzo
vya ndani,sh 360,000,000 ni fidia ya kodi na sh 807,526,190 ni ruzuku
toka serikali kuu.
Aidha sh 948,580,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida n ash
1,054,216,050 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sh 20,000,000 ni
wadau/wahisani wa maendeleo.
Home »
» HALMASHAURI NZEGA KUTUMIA BILIONI 35.4 2014/2015.
0 comments:
Post a Comment