Home » » PINDA AKABIDHI SH MILIONI 18.9 MRADI WA VIJANA SIKONGE.‏

PINDA AKABIDHI SH MILIONI 18.9 MRADI WA VIJANA SIKONGE.‏

Na Hastin Liumba,Sikonge
 
PINDA AKABIDHI SH MILIONI 18.9 MRADI WA VIJANA SIKONGE.
 
WAZIRI mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda
amekabidhi kiasi cha sh milioni 18.9 katika mradi wa vijana wa
Pathfinder Green City wilayani Sikonge mkoani Tabora.
 
Msaada huo alikabidhi baada kutoa ahadi yake pindi alipoutembelea na
kufurahishwa na namna kundi la vijana linavyotekeleza kazi mbalimbali
za miradi ya maendeleo.
 
Mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu alikabidhi msaada huo kwa
niaba ya waziri mkuu.
 
Selengu alikabidhi seti ya TV aina ya Samsung na Deki yake vyote
vikiwa na thamani ya sh 2,850,000,fedha taslimu sh milioni kumi na
5,900,000 kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki aina ya Bajaj vyote vikiwa
na thamani ya sh milioni 18,915,000.
 
Selengu alisema anakabidhi msaada huo kama kutimiza ahadi ya waziri
ambaye pindi alipotembelea mradi huo aliahidi aliyoyatekeleza leo.
 
“Leo nawakabidhi seti ya TV….lakini pia kuna kiasi cha sh milioni kumi
za ufugaji wa kuku wa kienyeji pamoja na kiasi sh milioni 5,900,000
fedha hizi bado zipo kwenye akaunti na vitu vitanunuliwa hivi pude kwa
leo pokeeni hii seti ya TV.”alisema.
 
Selengu alisema vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si
vinginevyo na kwamba serikali iko pamoja na vijana walioko kwenye
mafunzo hayo.
 
Mradi huo wa vijana wa Pathfinder Green City wenye vijana 100
wanajifunza na kutekeleza shughuli mbalimbali za kijasiliamali kama
ufugaji,kilimo,uashi ujenzi,ufugaji nyuki na urinaji asali na kilimo
cha bustani.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa