Home » » WALIOTEKA MAGARI WATUPWA JELA MIAKA 90

WALIOTEKA MAGARI WATUPWA JELA MIAKA 90

MAHAKAMA ya Hakim Mkazi wilaya ya Nzega mkoani Tabora imewahukumu watu watatu kwenda Jela miaka 90 kwa kubainika na kosa la Unyanganyi wa kutumia siraha kuwa pola Mill 18 ambapo ni kinyume na kifungu cha 287 cha sheria ya kanuni ya adhabu.
 
Akisoma Hukumu hiyo Hakim Mkazi Mfawidhi silvester kainda,baada ya kusikiliza ushahidi wa mashitaka kwa washitakiwa watatu kati ya watano,ushahidi umethibitisha bila kuacha shaka kuwa Antony Joseph,Charles Richard na Samweli John wamehukumiwa kwenda jela miaka 90 huku kila mmoja akitumikia miaka 30 jela.
 
Awari ya hapo Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polis mkaguzi msaidizi Mellito ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo April 2 mwaka 2013 watuhumiwa watano waliotuhumiwa kwa kuteka wafanya biashara walio kuwa wakienda mnadani mambali na kupola mill 18.
 
Ameiambia mahakama hiyo kuwa majambazi hayo yakitumia siraha aina ya Bunduki SMG 1 yalifanikiwa kupola fedha hizo za wafanya biashara.
 
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polis Mellito ukongoji aliwataja waliokamatwa na tukio hilo kuwa ni samweli John(35) mkazi wa nzega nyasa,Joseph kisumo,mkwangu masaniwa(30) mkazi wa ngukuno panoja na charles(25)nkazi wa kosangati kibondo kigoma na charles Richard mkazi wa kipilimuka.
 
Washitakiwa watatu kati ya watano wamekumbwa na hokum hiyo ya miaka 90 jela ambaoni ni Antony Joseph,Charles Richard na samweli John huku washitakiwa wawili wakiachwa huru baada ya kutobainika na hatia ya utekaji ambao ni Joseph Kisumo na mkwangu masaniwa.
 
Melito  ameiambia mahakama hiyo kuwa itoe adhabu kali iliiwefundisho kwao na kwa jamii hata hivyo washitakiwa hao watatu walipewa nafasi ya kujitetea hawakujitetea b adala yake waliiomba mahakama hiyo iwapatie nakala ya hokum zao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa