Home » » Halmashauri yaagizwa kutengeneza Magari yake

Halmashauri yaagizwa kutengeneza Magari yake

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imeagizwa kutengeneza Magari yake ili watumishi waanze kwenda kwa wananchi Vijijini.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mh.John Kadutu,alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo Mjini Kaliua.

Amesema watumishi kipindi hiki hawawezi kwenda kwa wananchi kusikiliza na kutatua kero zao kutokana na ukosefu wa magari ambayo ni mabovu na kuaagiza magari yote mabovu yawe yametengenezwa katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuanzia sasa.

Mwenyekiti huyo ametaka watumishi wote kufanya kazi zao kwa malengo na sio kufanya kazi kwa mazoea na kwamba wanatakiwa kueleza wamefanya mambo gani katika kipindi walichojipangia

Kwa upande wa mapato,Kadutu ameagiza kila Mkuu wa Idara awe katika nafasi ya kueleza jitihada alizofanya katika kukusanya mapato ya halmashauri kwenye Idara yake.

Amesema wakati umefika wa Halmashauri kuzidi kupanua wigo wa ukusanyaji mapato na sio kutegemea ushuru wa zao la Tumbaku peke yake.

Halmashauri ya wilaya ya Kaliua imeanzishwa baada ya kugawanywa Halmashauri ya wilaya ya Urambo ambayo inategemea zaidi ushuru wa zao la tumbaku ambalo ndio zao kuu la Biashara.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa