Na Hastin Liumba,Tabora
MRADI wa vijiji vya Millenia MVP (Mbola) wilayani Uyui mkoani Tabora,
umetoa vyandarua 640 kwa baadhi ya hospitali na vituo vya afya ikiwemo
hospitali ya rufaa Kitete zenye thamani ya sh milioni 4.8.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vyandarua hivyo katika
ofisi za mradi huo, kiongozi wa mradi Dk Gerson Nyadzi alisema neti
hizo ni katika na kudhibiti ugonjwa wa malaria kwenye vijiji vya
Millenia Mbola.
Dk Nyadzi alisema vyandarua hivyo zitagaiwa katika hospitali ya rufaa
Kitete vyandarua 240,kituo cha afya cha mtakatifu Ann Ipuli vyandarua
80,kituo cha afya mtakatifu Phillip vyandarua 40.
Aidha hospitali nyingine ni hospitali ya jeshi Milambo vyandarua 200
na kituo cha afya Upuge vyandarua 80 vyote vikiwa na thamani ya sh
milioni 4.8.
Dk Nyadzi alisema mradi huo umesadia kupunguza kasi ya ugonjwa wa
malaria kwa kugawa vyandarua vyenye viatilifu vipatavyo 25,000 mwaka
2007 vikiwemo vyandarua 24,000 vilivyogaiwa kwa wakazi wa eneo la
mradi.
Alisema jumla ya vyandarua 11,000 viligaiwa katika vijiji 11
vinavyozunguka eneo la vijiji 16 vilivyoko kwenye mradi .
Alisema mwaka 2012 jumla ya vyandarua 4,314 viligaiwa na mwaka 2013
mradi uligawa vyandarua 5,434 na hadi sasa wananchi wengi wameelewa
umuhimu wa kutibiwa na kutumia vyandarua.
Dk Nyadzi alisema mradi huo umeendelea kufanya kazi na serikali na
wadau wengine katika sekta ya afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa
katika usimamizi wa kazi mbalimbali kwa kuleta maendeleo ya kudumu
kwenye vijiji vinavyozunguka mradi.
Hata hivyo Dk Nyadzi alisema katika kupambana na malaria bado kumekuwa
na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa Vitendanishi vya kupimia Malaria
mRDT na vinginevyo.
Changamoto nyingine alisema ni kutokkuwepo kwa dawa za mseto kwa muda
mrefu,ufinyu wa bajeti katika kutekeleza kazi,uwemo wa imani potofu
kwa jamii juu ya matumizi ya vyandarua na jamii kutokutunza mazingira
yanayowazunguka.
Home »
» MRADI WA MILLENIA WATOA VYANDARUA VYA MIL 4.8.
0 comments:
Post a Comment