Home » » IGUWASA yabaini wanaoihujumu

IGUWASA yabaini wanaoihujumu

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka wilayani Igunga (IGUWASA) imefanikiwa kuwabaini  watu wawili waliojiunganishia maji kwa njia ya wizi

Kubainika kwa Watu hao  kunatokana na msako  unaoendeshwa na IGUWASA kwa lengo la kuwabaini wanaofanya  hujuma ya kuiba maji kwa  kujiunganishia wenyewe pasipo kufuata taratibu za Mamlaka.

Meneja wa IGUWASA,Raphael Melumba amesema watu hao walibainika kwa siku tofauti  na kuwataja majina kuwa ni Shela Mtao na  Nicholaus Marwa. Wote wakiwa ni wakazi wa  Mjini Igunga.

Amesema, watu hao walikutwa na wafanyakazi wa IGUWASA waliokuwa kwenye operesheni   ambapo Shela Mtao alikiri kufanya kosa  na kutozwa faini ya Shilingi 500,000 alizozilipa huku Nicholaus Marwa akikosekana nyumbani kwake ingawa ana kosa la kujiunganishia maji kinyume cha utartibu na kwamba anatafutwa

Ameeleza  kuwa zoezi hilo ni endelevu na kutoa onyo kwa wananchi wanaofikiria kujiunganishia maji kinyume cha sheria kuacha kuwaza hivyo kwani wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria

Siku chache zilizopita IGUWASA kupitia Meneja wake,alitangaza msako wa kuwabaini watu wanaoihujumu Mamlaka hiyo kwa kujiunganishia maji kinyume cha utaratibu na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa