Home » » KUNGUNI WASUMBUA WODI YA AKINAMAMA

KUNGUNI WASUMBUA WODI YA AKINAMAMA

WODI ya Akinamama katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani tabora inakabiliwa kuingiliwa na wadudu aina ya kunguni ambao wamekuwa kero kwa akinamama wanaokwenda kujifungua.


Wakizungumza kuhusu  kunguni hao baadhi ya akinamama katika hospitali hiyo wamesema wanatishia sio tu Afya zao bali hata za watoto wachanga wanaozaliwa na kulazwa katika Wodi hiyo.

Mkazi wa Mjini Igunga ambaye amejifungua hivi Karibuni na kulazwa kwenye Wodi hiyo,aliyejitambulisha kwa jina la Amina Rajab,amesema kunguni hao ambao wapo  katika Wodi ya akinamama wamekuwa wakiwawapa shida na kusumbua na kuwa kero kwa wazazi hao.


Kaimu Bwana Afya wa Wilaya ya Igunga,Paulo Mtumba amekiri kuwepo kwa Kunguni hao katika Wodi ya Akinamama ambayo ni Namba Moja  akisema  suwala hilo wanalitambua na wamekuwa wakilishughulikia ili kuweza kuepusha wagonjwa na usumbufu wa kunguni hao ambao wanaweza pia kuleta madhara kiafya kwa wanaotumia Wodi hiyo.


Amesema, pamoja na kushughulikia tatizo hilo pia inahitajika kutolewa Elimu  kwa wagonjwa, kwa kuwa Hospitali hiyo imekuwa ikipokea watu mbalimbali ambao wanatoka Mikoa jirani ambao  baadhi yao hawazingatii suala la usafi na kusababisha kuwepo kwa Kunguni hao.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Igunga ,Dk.Fidelis Mabula ameeleza kuwa  Uongozi  wa Hospitali utajadili kuwepo kwa Kunguni hao ili waone jinsi ya kutatua tatizo hilo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa