Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, amewataka wanawake
walioolewa wilayani humo kuwagomea waume zao endapo watakataa kulipa
fedha za kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Alisema mafanikio ya mgomo wa kina mama kwa wanaume wanaokataa
kuziunganisha familia zao na huduma ya CHF utawafanya wajiunge na
huduma hiyo ili kuwapa uhakika wa matibabu ya dharura pindi wanapokosa
fedha.
“Tunawahimiza wote kina baba na kina mama mjiunge na huduma hii na
kina mama ninyi na watoto wenu ndio waathirika wakubwa wa kukosa fedha
za matibabu kwa wakati.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment